ZIARA YA NAIBU WAZIRI WA HABARI, MAWASILIANO NA TEKNOLOJIA YA


ZIARA YA NAIBU WAZIRI WA HABARI, MAWASILIANO NA TEKNOLOJIA YA HABARI KATIKA MKOA WA KIGOMA

Na,Simon Kibarabara-Kigoma

Naibu Waziri wa  Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe.Mhandisi Kundo Andrea Mathew (Mb) Leo tarehe 11.01.2024 anaendelea na ziara yake katika Mkoa wa Kigoma ya kukagua miradi ya Mawasiliano inayo tekelezwa katika Mkoa huo .

Naibu Waziri Kundo, amekagua ujenzi wa mnara wa Halotel katika Kijiji cha Bunyambo kata ya Bunyambo wenye thamani ya Shilingi milioni 250, ujenzi wa Mkongo wa Taifa Buhigwe wenye thamani ya Shilingi 953,741,765.68, pamoja na ujenzi  wa mnara wa Airtel katika Kijiji cha Mwakizega Kata ya Mwakizega wenye thamani ya Shilingi Milioni 250.

Aidha, Mhe. Naibu Waziri Kundo amewaeleza wananchi wa Kigoma kuwa Serikali ya awamu ya Sita inayo ongozwa na Mhe. Rais Dkt.  Samia Suluhu Hassan inaendelea  na  jukumu la kuhakikisha huduma za mawasiliano zinapatikana kwa urahisi nakusema kuwa Serikali  ipo katika mchakato wa mwisho wa kupata fedha kwa ajili ya ujenzi wa minara 636 na minara 15 itajengwa katika maeneo ya mipaka kwa ajili ya kuboresha usikivu wa Radio na minara 621 itajengwa kwa ajili ya kutoa huduma za mawasiliano ya simu Nchi nzima.

Naibu Waziri Kundo akizungumza na wananchi wa Buhigwe ameeleza kuwa Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ametoa pesa kiasi cha Shilingi milioni 277 kwa ajili ya ujenzi wa kilometa 55 zinazojumuisha kilometa 18 kutoka Mayovu na kilometa 37 kutoka Kasulu 

Vile vile, Naibu Waziri  Kundo amewaeleza wananchi wa Buhigwe kuwa Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ametoa Bilioni 170 kwa ajili ya ujenzi wa kilomita 4,442 na vituo 111 Vya Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano Nchini. Kiasi hiki kinajumuisha Bilioni 7.28 iliyotumika kununua magari 45 yatakayo saidia katika utekelezaji wa huduma za Mkongo Nchini.

Kwa upande wake,  Meneja wa TTCL Mkoa wa Kigoma Eng. Aman Kichele ameeleza kuwa ujenzi wa kituo Cha Mkongo wa Taifa cha Buhigwe kitasaidia kuboresha huduma za mawasiliano kwa wananchi, kukuza biashara na kuongeza vipato kupitia biashara mtandao, kupata huduma za Afya kwa njia ya Mtandao, kushuka kwa gharama za mawasiliano, kuchangia mapato ya Serikali pamoja na kuimarisha usalama wa wilayani, Mkoa na Nchi Nzima kwa ujumla.

Sambamba na hayo,  Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Buhigwe Eng.Erineo January ameishukuru sana Serikali ya Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kutekeleza Ilani ya Chama Cha Mapinduzi katika Mkoa huo wa Kigoma, na kushukuru kwa miradi ya Mawasiliano ambayo imeletwa katika Mkoa wa Kigoma .

Post a Comment

Previous Post Next Post