WAZIRI MAVUNDE AKABIDHI MAGARI 25 KWA TUME YA MADINI

WAZIRI MAVUNDE AKABIDHI MAGARI 25 KWA TUME YA MADINI 

Na,Saleh Lujuo-Dodoma

Waziri wa Madini Mhe.Anthony Mavunde amekabidhi jumla ya magari 25 kwa  Tume ya Madini ili kuboresha utendaji kazi na kuongeza ukusanyaji wa maduhuri huku akitoa rai kwa watumishi watakaokidhiwa magari hayo kuhakikisha wanayatumia ipasavyo na kuweze kufikia lengo lililokusudiwa.

Waziri Mavunde ameyasema leo Oktoba 21 2024 jijini Dodoma wakati wa hafla ya uzinduzi wa magari hayo na kuongeza kuwa  jumla ya Bilioni 18 zimetengwa kwa ajili ya ununuzi wa magari na pikipiki.

Amesema katika mwaka huu wa fedha wizara ya madini imepangiwa kukusanya sh.trilioni moja hivyo vitendea kazi hivyo vitasaidia katika kufikia lengo.

“Magari haya 25 yanaenda kuongeza kasi ya ukusanyaji wa mapato katika  mikoa ya kimadini na katika mwaka huu wa fedha katika kipindi cha siku 90 tumekusanya sh. bilioni 287 ikiwa tumevuka lengo la kukusanya sh.bilioni 241 katika kipindi tajwa,”amesema

Ameongeza kuwa bajeti ya wizara ya madini imeongezeka kutoka sh.bilioni 89 mwaka 2016 hadi kufikia sh.bilioni 231 mwaka huu. Jukumu tulilonalo ni kuhakikisha sekta hii ya madini inatoa mchango chanya katika ustawi wa uchumi wa Taifa kwa kuhakikisha tunaongeza kiwango cha makusanyo.

Katika hatua nyingine Mavunde amesisitiza kuwa magari hayo yatafungwa vifaa maalumu vya kuyafuatilia ili yasitumike vibaya.

Kwa upande Kaimu Mtendaji Mkuu wa Tume ya Madini Mhandisi Ramadhani Lwamo amesema serikali imekuwa ikiongeza bajeti kwa wizara ili kuhakikisha kunakuwa na vitendea kazi vya kutosha.

Amefafanua kuwa vifaa hiovyo vitasaidia kuongeza kasi ya ukusanyi mapato ili kuongeza makusanyo ya serikali.

“Wizara imekuwa na bajeti ya kutosha leo hii tumepokea magari 25 ambayo yatasaidia kuongeza ufanisi katika utekeleza ji wa majukumu. Vitendea kazi hivi vitasaidia Maofisa madini wakazi wa mikoa kufuatilia shughulimbalimbvali za madini katika maeneo yao,”amesema

Kwa upande wake Ofisa Madini Mkazi wa Mererani Nchangwa Marwa ameipongeza serikali ya Awamu ya sita chini ya uongozi wa Rais Dk.Samia kwa kuendelea kutoa ffedha kwa ajili ya kuboresha utendaji kazi.

Amesema vifaa hivyo vitasaidia kuongeza kasi ya ufuatiliaji wa maduhuli ya serikali na kufika maeneo mengi ambayo ilikuwa ni ngumu kufikika.

“Changamoto ya vitendea kazi ilikuwa inakumba maeneo meneo mengi tunaishukuru serikali na tunaamini vitaenda kuongeza chachu na kasi ya ufuatiliaji wa maduhuli ya serikali,”amesema









Post a Comment

Previous Post Next Post