WAFANYABIASHARA WAASWA KULIPA KODI


WAFANYABIASHARA WAASWA KULIPA KODI

Na. Wellu Mtaki, Dodoma 

Mamlaka ya mapato Tanzania (TRA ) imewasihi wafanyabiashara  kuendelea kulipa kodi kwa hiari ili kuepukana na riba pamoja na adhambu mbalimbali zitokanazo na ukwepaji wa kulipa kodi Sambamba na kusaidia kukuza uchumi wa nchi.

Rai hiyo imetolewa  jijini Dodoma  na Kamishina mkuu wa mamlaka ya mapato Tanzania Yusuphu Juma Mwenda wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mafanikio na mwelekeo wa mamlaka hiyo katika kuelekea maadhimisho ya miaka minne ya serikali ya awamu ya sita chini ya Mhe.Dkt.Samia Suluhu Hassan Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania.

Amesema Moja ya mambo yanayosaidia kukuza uchumi wa nchi ni pamoja na ulipaji Kodi kwani maendeleo ya nchi yanatokana na Kodi .

Aidha  amewahakikishia watanzania ya kuwa mamlaka hiyo itaendelea kutekeleza maagizo Mhe.Rais  ikiwemo  mfumo wa kodi unaotabirika,wenye usawa,unaotenda haki kwa kila mmoja na unaowezesha kukua kwa biashara sambamba na kuendelea kuimarisha ushirikiano na viongozi wa wafanyabiashara.

Pia amesema miongoni mwa mafanikio waliyoyapata katika kipindi cha miaka minne ya serikali ya awamu ya sita nipamoja na  Kuimarisha Weledi na Uadilifu wa Watumishi wa mamlaka hiyo na kuchukua hatua kwa mujibu wa sheria kwa wachache wanaokiuka maadili ya utumishi wa umma ambapo imewachukulia hatua baadhi ya watumishi wanaoenda kinyume na maadili kwa kuwafukuza kazi watumishi 14,kuwashusha mishahara watumishi 6,kuwashusha cheo na kuwapunguzia mishahara watumishi 6 na kuwapa onyo la maandishi watumishi 22.

Ikumbukwe kuwa kila  mfanyabiashara anatakiwa  kutoa Risiti za kielektroniki (EFD)kila wanapouza bidhaa na huduma mbalimbali na kuwasilisha ritani za kila mwezi na Kuhakikisha hawajiingizi katika ununuzi wa risiti za EFD bandia .

Post a Comment

Previous Post Next Post