VIFAA TIBA VYA KUCHAKATA SAMPULI ZA MAABARA TAKRIBANI 2, 500 KWA SIKU VYAONGEZWA


VIFAA TIBA VYA KUCHAKATA SAMPULI ZA MAABARA TAKRIBANI 2, 500 KWA SIKU VYAONGEZWA

Na,Wellu Mtaki-Dodoma

Serikali imeongeza vifaa tiba vyenye uwezo mkubwa wa kuchakata sampuli za maabara takribani 2,500 kwa saa moja ili kuongeza upatikanaji haraka wa majibu na kupata matibabu mapema kwa wagonjwa wa nje waliolazwa.  

Hayo yamesemwa  na Mkurugenzi huduma ya Upasuaji Muhimbili, Dkt.Rachel Mhavile amesema hayo wakati wa kutoa taarifa ya mafanikio kwa miaka minne ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan kwa waandishi wa habari katika ukumbi wa Habari Maelezo Jijini Dodoma

Vifaa hivyo vina thamani ya TZS. 1.8 Bil. Upatikanaji wa vifaa hivyo umerahisisha utoaji wa majibu kwa haraka, magonjwa kugundulika haraka, kupunguza muda wa wagonjwa kusubiri matibabu na kuwezesha upatikanaji wa huduma za kibobezi ikiwemo upandikizaji mimba (IVF), upandikizaji figo na uloto

Aidha amesema kuwa hospital ya Taifa Muhimbili (MNH), imeanzisha huduma ya kuvuna mifupa ya mbavu na nyonga kwa ajili ya kutengeneza taya ya chini ambapo gharama yake itakuwa Sh.Milioni 6.2.

Amesema  huduma hiyo ni mpya katika hospitali za Umma nchini na itasaidia kuimarisha taya ya chini, mifupa hiyo itavunwa kwa mgonjwa mwenyewe baada ya kufanyiwa vipimo na kuona ni jinsi gani inafaa.

Akitoa ufafanuzi juu ya mifupa hiyo amesema kuwa mifupa itavunwa kwa mgonjwa mhusika anayetaka huduma ya kutibiwa taya na pindi atakapokuwa amepatiwa matibabu itakuwa moja kwa moja na siyo ya kutoa na kurejesha.

Pia amesema huduma hiyo itasaidia kutengeneza mizizi bandia ya meno ambayo nayo atawekewa mgonjwa , pia mgonjwa hatapata usumbufu wa kubadilisha mizizi hiyo au taya.

Aidha amesema kuwa kwa sasa watoto 54 wamefanyiwa upasuaji na kuwekewa vifaa vya kuwasaidia kusikia kwa gharama ya Sh.  bilioni 2.3 kwa wote na kusaidia kuokoa kiasi cha shilingi Bilioni nne kama wangeenda kutibiwa nje ya nchi.

Post a Comment

Previous Post Next Post