ZAIDI YA BILIONI 11.8 ZAPOKELEWA NA BUWSSA
Na,Wellu Mtaki-Dodoma
Mamlaka ya maji safi na usafi wa Mazingira Bunda (BUWSSA) imepitishiwa miradi ya thamani ya TShs zaidi ya Bilioni 28.1 ambapo kiasi cha zaidi Tshs Bilioni 11.8 tayari zimepokelewa na baadhi ya miradi imekamilika na mingine utekelezaji wake unaendelea.
Ameyasema hayo Mkurugenzi Mtendaji wa ya majisafi na usafi wa Mazingia Bunda Esther Gilyoma wakati akizungumuza na waandishi wa habari jijini hapa Dodoma kuhusu mafanikio na mwelekeo wa mamlaka hiyo kuelekea maadhimisho ya miaka minne ya serikali ya awamu ya sita ambapo amesema kuwa tayari wamekwisha zifikia kata 12 na mbili zinaendelea kupatiwa huduma.
Amesema mamlaka ya BUWSSA itahakikisha huduma ya maji inaendelea kuimarika katika mji wa Bunda kwa mwaka wa Fedha 2025/2026 ambapo wanampango wa ujenzi wa tenki kubwa la maji kwenye mwinuko wa mita 1537 mlima nyiendo wenye uwezo wa kubeba lita 5,000,000 ili kuwa na uwezo wa kuhifadhi maji pindi umeme unapo katika.
Aidha amesema Kwa mwaka 2021 Mamlaka ilikuwa inatoa huduma ya maji kwa wastani wa masaa 12 kutokana na ufinyu wa mtandao na kutakuwa na maji ya kutosha,kwa mwaka 2023 baada ya mradi mkubwa wa kusafisha na kutibu maji Nyabehu Bunda kukamilika.
