MAFUNZO YA ITIFAKI NA USTAARABU WA KIDIPLOMASIA NI MUHIMU KATIKA UTOAJI HUDUMA-RC SENYAMULE
Na,Saleh Lujuo-Dodoma
Kutokana na umuhimu wa itifaki na ustaarabu wa kidiplomasia katika jamii hapa nchini, taasisi ya protocol service team (PST) imedhamiria kutoa mafunzo nchi nzima kwa lengo la kuboresha uelewa katika Masuala ya itifaki na ustaarabu wa kidiplomasia.
washiriki kutoka mikoa 19 ya Tanzania Baraza na visiwani wamepatiwa mafunzo hayo ili kujengewa uelewa wa namna bora ya kuongeza heshima katika Kutoa huduma mbalimbali kwenye hafla zinazofanyika hapa nchini.
Akifunga Mafunzo ya itifaki na Ustaarabu wa kidiplomasia leo January 26,2025 jijini Dodoma yaliyoratibiwa na Taasisi ya Protocol Service Team(PST), Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Rosemary Senyamule amewasisitiza washiriki wa mafunzo hayo kwenda kuwa mabalozi katika kufikisha Elimu waliyopata kwa makundi mengine ili nao wafahamu umuhimu wa mafunzo hayo.
"mmejifunza,kaoneaheni kwa vitendo mlichojifunza na elimu mpya mliyopata nendeni kaoneaheni kwa wengine ili nao wajifunze katika kulitumikia Taifa lao na huu ndio utaifa wenyewe". Amesema.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa PST Tanzania Hussein Abubakari Hussein ameeleza kuwa Mafunzo haya yalilenga kuboresha uelewa masuala ya Itifaki na Ustaarabu wa Kidiplomasia kwa Washiriki kutoka Sekta mbalimbali hapa nchini.
"Mafunzo haya yalilenga kuboresha uelewa wa masuala ya Itifaki na Ustaarabu wa Kidiplomasia kwa washiriki kutoka sekta mbalimbali, tunafurahi kuona washiriki kutoka Mikoa 19 kwa Bara na Visiwani wakiwa wamejifunza somo hili muhimu". Amesema.
"mafunzo haya yamehusisha washiriki kutoka makundi mbalimbali ikiwa ni pamoja na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Dodoma, Morogoro, Singida, Iringa na viongozi wa Dini pamoja na walimu". Ameongeza
Taasisi ya Protocol Service Team(PST) itaendelea kutoa Mafunzo ya itifaki na ustaarabu wa kidiplomasia kwa taasisi Mbalimbali ili kuboresha uelewa katika namna sahihi ya kutoa huduma.




