SERIKALI IMEJIPANGA KUTOKOMEZA MAGONJWA YA MIFUGO NCHINI-DKT. KIJAJI
Na,Saleh Lujuo-Dodoma
Serikali kupitia wizara ya mifugo na uvuvi imedhamiria kutokomeza magonjwa ya Mifugo na Kupunguza athari za ugonjwa wa kideriKwa kuku na jamii nyingine ya ndege ili kuongeza uzalishaji pamoja na kuwezesha Biashara ya mifugo na mazao yake ndani na nje ya nchi.
Kauli hiyo ya serikali ameisema waziri wa Mifugo na Uvuvi Dkt. Ashatu Kijajia leo Disemba 18,2024 katika kikao kazi Cha Uzinduzi wa uhamasishaji wa chanjo za mifugo Kitaifa ambapo amesema changamoto ya kuchanja mifugo kidogo kidogo kwenye mamlaka za Serikali za mitaa na hata kwa mfugaji mmoja mmoja ndiyo chanzo cha kushindwa kuleta tija ya kutokomeza magonjwa ya mifugo hapa nchini.
Kadhalika,Dkt. Kijaji amesema serikali imekuwa ikifanya jitihada mbalimbali za kuwasaidia wafugaji kufuga kwa tija na lengo la serikali ni kupanua wigo wa kuuza mifugo na nyama nje ya nchi pamoja na maisha ya wafugaji kuboreka.
Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (wa pili kushoto), akisalimiana na Mwenyekiti wa Chama cha Wafugaji Tanzania, Ndg. Mrida Mshota (wa kwanza kulia), mara baada ya kuwasili kwenye Uzinduzi wa Uhamasishaji wa Kampeni ya Chanjo za Mifugo Kitaifa katika Ukumbi wa Jakaya Kikwete, Disemba 18, 2024 Dodoma.
Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Prof. Riziki Shemdoe, akizungumza na wadau wa Mifugo, ni katika Uzinduzi wa Uhamasishaji wa Kampeni ya Chanjo za Mifugo Kitaifa katika Ukumbi wa Jakaya Kikwete, Desemba 18, 2024 Dodoma.
Mkurugenzi wa Huduma za Mifugo Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Dkt. Benezeth Lutege Malinda, akitoa utangulizi na utambulisho wa wadau mbalimbali wa Mifugo, ni katika Uzinduzi wa Uhamasishaji wa Kampeni ya Chanjo za Mifugo Kitaifa, uliofanyika katika Ukumbi wa Jakaya Kikwete, Desemba 18, 2024 Dodoma.
Ikumbukwe kuwa Tanzania ni moja ya nchi barani Afrika yenye mifugo mingi na hivyo kufanya uwezo wa kuchangia sana katika pato la Taifa ambapo kauli mbiu ya kikao kazi hicho Cha Uzinduzi wa uhamasishaji wa chanjo za mifugo Kitaifa unasema kwamba "Tokomeza magonjwa ya mifugo ili kuongeza uzalishaji na kuwezesha Biashara ya mifugo na mazao yake ndani na nje ya nchi.




