SERIKALI YA TANZANIA IMEKIRI KUPOKEA BILLION 240 KUTOKA SERIKALI YA CANADA KWA AJILI YA SEKTA YA AFYA.

SERIKALI YA TANZANIA IMEKIRI KUPOKEA BILLION 240 KUTOKA SERIKALI YA CANADA KWA AJILI YA SEKTA YA AFYA.

Na,Saleh Lujuo-Dodoma

Katika jitihada mbalimbali za kuboresha na kuimarisha huduma za Afya nchini, serikali ya Tanzania imekiri kupokea Billion 240 kutoka serikali ya Canada na kati ya fedha hizo shilling Billion 140 zitaingia moja kwa moja serikalini kwa ajili ya kuchangia Mfuko wa Afya wa pamoja.

Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu  amekiri kupokea Fedha hizo leo julai 20,2023 jijini Dodoma, kupitia kwa waziri wa maendeleo ya kimataifa na waziri Mwenye dhamana ya shirika la maendeleo ya uchumi la pasifiki la Canada Mhe.Harjit sajjan ambapo ameishukuru Serikalia ya Kanada kwa kutoa msaada huo.

Waziri Ummy amesema kati ya kiasi hicho kilichotolewa shilingi  Billion 140 zitaingia serikalini kwa ajili ya kuchangia mfuko wa afya wa pamoja ambapo mpaka sasa Serikali ishapokea kiasi cha shilingi Bilioni 94 ambazo zimeelekezwa kwenye akaunti za ngazi ya msingi ambazo ni zahanati, vituo vya afya na hospital za wilaya.

"Mfuko wa Afya wa pamoja ndiyo Mhimili mkubwa WA utoaji wa huduma za Afya katika ngazi ya Msingi ikiwemo zahanati,vituo vya Afya na hospital za WILAYA". amesema. 

“Kwa ujumla mchango wa Serikali ya Kanada kwa Tanzania umeleta matokeo mazuri kwa Huduma za afya Tanzania leo tunaongea wanawake karibu asilimia 90 wajawazito wanajifungulia katika vituo vya kutolea Huduma za afya kwa sababu ya mchango wa Kanada”. ameongeza


Waziri Ummy amesema fedha hizo zitajikita katika mambo makubwa matatu ikiwemo Afya ya uzazi,  mama,watoto wachanga na vijana ambapo fedha zingine zitaenda Kwa wadau wengine wakiwemo WHO, UNICEF, Plan international Canada,Nutrition International na World vision Tanzania.

Sambamba na hayo,waziri Ummy amesema kupitia msaada wa serikali ya Canada umesaidia kupunguza vifo vya watoto wenye umri chini ya miaka 5 kutoka vifo 67 katika kila vizazi hai 1000 hadi vifo 43. 

“Lakini pia tumeweza kupunguza mimba za utotoni kutoka asilimia 27 hadi asilimia 22 , tumepunguza udumavu kutoka asilimia 38 na sasa tunazungumzia asilimia 31 na kwa watoto wetu wanapata chanjo”, amesema waziri Ummy.

Kwa upande wake Waziri wa Maendeleo ya Kimataifa wa Kanada Mhe. Harjit Sajjan amesema kuwa wametangaza miradi mitano mipya ya afya yenye thamani ya dola za Canada milioni 128.5 ambapo dola za Canada milioni 75 kwa mfuko wa ruzuku wa shughuli za Mfuko wa Afya wa Pamoja (Health Sector Busket Fund, HSBF)  kwa serikali ya Tanzania na nyongeza ya dola za Canada 500,000  kwa UNICEF kwa usaidizi wa kitaalam.

"Leo nina furaha pia kutangaza dola za Canada milioni 23 katika ufadhili wa shirika la CanGIVE kwa miradi miwili mipya kwa ushirikiano na UNICEF Tanzania na shirika la Afya Duniani,Tanzania miradi hii ya CanGive itasaidia juhudi za watanzania kuchanja makundi yaliyopewa kipaumbele kwa njia ambayo itaimarisha huduma za afya kwa mapana zaidi”,  Amesema Mhe.Sajjan

Serikali ya Canada imeweka ahadi ya miaka 10 katika kuendeleza huduma za Afya na haki za wanawake na wasichana ulimwenguni kote.

Post a Comment

Previous Post Next Post