RAIS DKT. SAMIA SULUHU HASSAN KUONGOZA MADHIMISHO YA SIKU YA KUMBUKUMBU YA MASHUJAA

RAIS DKT. SAMIA SULUHU HASSAN KUONGOZA MADHIMISHO YA SIKU YA KUMBUKUMBU YA MASHUJAA

Na,Saleh Lujuo-Dodoma.

RAIS Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuongoza maadhimisho ya siku ya kumbukumbu ya Mashujaa ambayo kwa mara ya kwanza yanafanyika katika Uwanja mpya na wa kudumu wa Mashujaa uliopo Mtumba Jijini Dodoma.

Ukamilikaji wa uwanja huo ni utekelezaji wa maono na maagizo yake aliyoyatoa Julai 25, mwaka jana katika kumbukumbu ya Mashujaa ambapo aliagiza kuwa na uwanja unaojitegemea na mkubwa kwa ajili ya mashujaa wetu.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Julai 29,2023 Ofisini kwake Jijini Dodoma,Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Rosemarry Senyamule amesema maandalizi hayo yamekamilika kwa asilimia 100.


"Julai 25 ya kila mwaka Tanzania huwa inaadhimisha kumbukumbu ya siku ya Mashujaa waliopoteza maisha yao wakiutetea, kuupigania na kuulinda Uhuru wa Nchi yetu. Siku hii ni muhimu kwa sababu inatukumbusha kuhusu wajibu wetu wa kutunza historia ya Mashujaa waliopigania, kutetea na kulinda Uhuru wa Nchi ya Tanzania ili kurithisha vizazi vijavyo umuhimu wa kutumia historia hii kukuza na kuendeleza amani na mshikamano wa kitaifa bila kujali tofauti mbalimbali, ikiwemo za kikabila, kidini na itikadi za kisiasa". amesema.

Hata hivyo,amewaomba watanzania kutafsiri ujasiri uliofanywa na mashujaa na kutumia maadhimisho hayo na kuimarisha umoja wa kitaifa huku akitoa wito kwa wananchi wa Mkoa wa Dodoma na Mikoa jirani kushiriki hafla ya Maadhimisho ya kumbukizi ya siku ya Mashujaa.


Maadhimisho hayo yataambatana na gwaride na matukio mbalimbali ikiwemo gwaride la jeshi,ambapo Julai 24, mwaka huu kuamkia Julai 25 Mkuu wa Mkoa wa Dodoma atawasha Mwenge wa mashujaa kwa niaba ya wana Dodoma na utazimwa na Mstahiki Meya wa Jiji la Dodoma Julai 25,mwaka huu saa sita usiku.

Post a Comment

Previous Post Next Post