Na,Saleh Lujuo-Dodoma
Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) imewataka wafanyabiashara nchini kuchangamkia fursa ya kujisajili kwani wasio na usajili hawatoweza kuomba tenda rasmi ambazo zinatangazwa na Taasisi mbalimbali za Serikali pamoja na huduma za kibenki.
Kauli hiyo ameitoa Afisa usajili wa wakala wa usajili wa Biashara na leseni (BRELA) Gabriel Girangay katika Madhimisho ya wiki ya utumishi wa umma ambayo Kitaifa yanafanyika jijini Dodoma.
Amesema Sheria ya BRELA inamtaka Kila mfanyabiashara ajirasimishe na ni vema Wafanyabiashara wakaona umuhimu wa kurasimisha biashara zao kwa kusajili BRELA na kupata leseni inayostahili ili waweze kuchangamkia fursa za kibiashara.
"Rasimisheni Biashara zenu mtapata faida nyingi mana Kuna watu wanatoka nje ya nchi anakuja Tanzania na anachokifanya anamtafuta mtu ambaye amesajiliwa ili aungane naye katika kuendesha Biashara zake,hivyo changamkieni hizi fursa kwa maslahi yenu binafsi na Taifa kwa ujumla". Amesema Girangai.
Girangay amesema kusajili Biashara kutawasaidia wafanyabiashara kupata ulinzi wa kisheria pamoja kuwawezesha kutambulika na Mataifa mengine yanapokuja hapa nchini.
“Tunajua moja ya malengo ya BRELA ni kuhakikisha zile biashara zisizorasmi zinarasimishwa, ni wazi kuwa mtu anayefanya biashara ambayo siyo rasmi kuchangia kwenye maendeleo ya taifa ni ngumu ndio maana tunaendelea kuwahimiza wafanyabiashara kurasimisha biashara zao,”. amesema
Sambamba na hayo Girangay ametoa wito kwa wakazi wa Jiji la Dodoma na maeneo ya jirani kufika katika Banda la BRELA ili wapate ufafanuzi zaidi wa kisheria na waweza kurasimisha Biashara zao kwani kufanya hivyo ni kuunga mkono Jitihada za serikali katika kukuza uchumi.
Kwa upande wake Meneja Rasilimali na utawala BRELA Migisha Kahangwa amesema wamekuwa wakitioa elimu kwa Wananchi kutumia huduma za BRELA na hivyo Ni muhimu wachangamkie Fursa ya elimu kupitia maonyesho hayo ya wiki ya Utumishi wa Umma kupata Elimu kuhusiana na huduma wanazozitoa.
Maadhimisho ya Wiki ya utumishi wa umma kwa mwaka 2024 yanafanyika Kitaifa Jijini Dodoma yakiongozwa na kauli mbiu isemayo "kuwekeza Kwa utumishi wa umma wa Africa karne yae21 iliyo jumuishi na inayostawi; ni safari ya mafunzo na mabadiliko ya kiteknolojia.