BILLION 3.5 ZIMETOLEWA NA MEDA KUPITIA MRADI WA FEGGE ILI KUZIFIKIA BIASHARA NDOGO NA KATI ZIPATAO 211 NCHINI
Na,Saleh Lujuo -Dodoma
Wizara ya Viwanda na Biashara imewasisitiza wafanyabiashara nchini kurasimisha biashara zao ili kuweza kuleta maendeleo na kukuza uchumi pamoja na kuongeza pato la Taifa.
Hayo yamesemwa leo Juni 26,2024 na Kaimu katibu mkuu wizara ya viwanda na biashara Saidi Msabimana katika ufunguzi wa mahafali ya wajasiriamali waliofuzu mafunzo ya kukuza Biashara kwa mwaka 2024 ambayo yametolewa na shirika la Kimataifa la maendeleo ya kiuchumi MEDA ambapo amesema ili uchumi wa nchi uweze kukua unahitaji biashara kuongezwa thamani katika mazao ya chakula ili kuleta tija.
"ili wafanya Biashara mfaidike na Fedha zinazotolewa na serikali lazma mrasimishe Biashara zenu ziweze kutambulika na iwe rahisi serikali kuwawezesha kukuza Biashara zenu ". Amesema
"na haya yote wanayofanya MEDA ni kuwaongezea ujuzi katika kuongeza ubora wa bidhaa mnazozalisha". Amesema
"na fursa hizi za mafunzo Mbalimbali ya kielimu zinazotolewa na wadau Mbalimbali wakiwemo MEDA dhamira yake ni kuwajengea uwezo namna Bora ya kukuza Biashara zenu". Ameongeza
Aidha, amelipongeza shirika la Kimataifa la maendeleo ya kiuchumi MEDA kwa mahafali ya wajasiriamali waliofuzu mafunzo ya kukuza biashara kwa mwaka 2024 ambapo washiriki 127 wamefuzu mafunzo hayo.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkaazi wa MEDA Tanzania Musa Lubango amesema MEDA kupitia Mradi wa FEGGE umeweza Kutoa kiasi cha shillingi Billioni 3.5 ili kuzifikia biashara ndogo na kati zipatao 211 ambapo 177 zimepatiwa Elimu ya kukuza biashara na 34 zimepatiwa ruzuku ya kuchangia.
"Mradi unachangia Asilimia 50 na wajasiriamali wanachangia Asilimia 50 na mradi umeshatoa ruzuku na Mafunzo kwa wakulima zaidi ya Elfu kumi wakiwa wanawake". Amesema
Naye Bi. Hellen Fytche ambaye ni kansela Mkuu wa ushirikiano na maendeleo kutoka ubalozi wa Canada ametumia fursa hiyo kuwapongeza wajasiriamali ambapo amewasihi kutumia Elimu waliyopata ili wafanikiwe kibiashara na kuleta mabadiliko chanya katika niashara zao.
"Mafanikio yenu ni zaidi ya hatua binafsi na yanatengeneza njia kwajili ya kesho yenu yenye mwangaza kwa jamii zenu na Tanzania kwa ujumla". Amesema.
Wahitimu 127 wamefuzu mafunzo ya kukuza Biashara kwa mwaka 2024 ambayo yametolewa na shirika la Kimataifa la maendeleo ya kiuchumi MEDA.