UCHAMBUZI WA ACT WAZALENDO NI UCHAMBUZI WA KITAIFA ZAIDI KULIKO UCHAMBUZI WA CHADEMA.

UCHAMBUZI WA ACT WAZALENDO NI UCHAMBUZI WA KITAIFA ZAIDI KULIKO UCHAMBUZI WA CHADEMA.

Na,saleh Lujuo-Dodoma.

Mbunge wa Mvumi Livingstone Lusinde amekemea kauli zinazotolewa na baadhi ya wanasiasa ambazo zinapotosha na kuleta ubaguzi katika Taifa huku akiipongeza serikali kwa dhamira ya uwekezaji katika eneo la Bandari ya Dar es salaam.

faida za uwekezaji huo ni kuongezeka kwa fursa za ajira,kupungua kwa urasimu wa kuchelewa kwa mizigo na kuongeza mapato ya bandari kutoka trilioni 7.7 hadi kufikia Ttrilioni zaidi ya 20.

Akizungumza na wandishi habari leo Alhamisi Juni 8,2023 jijini Dodoma,Mbunge huyo ambaye ni mjumbe wa Halmashauri kuu ya CCM(NEC), amesema kauli aliyetoa Mbowe  kuhusu bandari ya Dar es salaam ni kauli ya kibaguzi.

“Mbowe anayesema Rais na Waziri wanaotoka Zanzibar, ila bandari ni ya Dar es salaam. Hii inaweza ikaharibu Muungano, haya ni maneno yasiyo na uungwana, kwani anataka kutuaminisha ni kosa Rais na waziri kutoka Zanzibar. Huo ni ubaguzi.

“Hivi Rais akitoka Kilimanjaro mipaka yake ya kutoa uamuzi ihusu milima tu? Vitu vingine visiguswe, asizungumze kuhusu korosho azungumzie Kilimanjaro tu? Haiwezekani?” amesema Mbunge huyo.

Sambamba na Hayo Lusinde amesema uchambuzi uliofanywa na ACT WAZALENDO ni uchambuzi wa kitaifa zaidi na wenye nia njema kuliko uchambuzi aliyechambuwa Mbowe.

Hata hivyo,Lusinde amewashauri wanasiasa na wachambuzi kuacha kutumia lugha za kibaguzi katika kupinga baadhi ya mambo yanayofanywa na Serikali kwani bila kuchukua tahadhari Taifa linaweza kuingia kwenye migogoro.

Post a Comment

Previous Post Next Post