WATUMISHI SEKTA YA KODI WAMETAKIWA KUFANYA KAZI KWA WELEDI NA KUEPUKA VITENDO VYA RUSHWA.
Na, Saleh Lujuo-Dodoma.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango anayeshughulikia Mipango na Fedha Jenifa Omolo amewataka watumishi sekta ya Kodi kufanya kazi kwa Weledi na Kuepuka vitendo vya Rushwa ili kufikia Azma ya serikali ya kuwaletea wananchi maendeleo.
Omolo ametoa kauli hiyo Jijini Dodoma wakati akifungua mafunzo kwa Wahasibu kutoka sekta mbalimbali za umma yaliyolenga kuwaongezea uwelewa wa mifumo mipya ya ulipaji kodi ambapo amewataka kuzingatia Maadili katika utekelezaji wa Majukumu yao.
"fanyeni kazi kwa weledi na kujituma pamoja na kuepuka vitendo vya Rushwa ili tufikie azma ya serikali ya kuwaletea wananchi Maendeleo" amesema Omolo.
Sambamba na Hayo Omolo amewataka wahasibu hao kuzingatia sheria na kanuni ili kutekeleza majukumu yao ipasavyo.
Mafunzo hayo yanatarajiwa kutoa muarobaini wa kuwezesha ulipaji kodi kwa hiari kwa wafanyabiashara na kukndoa baadhi ya sintofahamu katika mchakato huo.