WANAFUNZI 188,128 WALIOKIDHI VIGEZO WACHAGULIWA NA KUPANGIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA TANO

WANAFUNZI 188,128 WALIOKIDHI VIGEZO WACHAGULIWA NA KUPANGIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA TANO

Na,Mwandishi wetu-Dodoma

Wanafunzi 188,128 waliokidhi vigezo wamechaguliwa na kupangiwa kujiunga na kidato cha tano katika shule mbalimbali nchini pamoja na vyuo vya fani mbalimbali.

Matokeo ya mtihani wa kidato cha nne mwaka 2022 yanaonyesha kuwa watahiniwa 192,348 walipata ufaulu wa daraja la kwanza hadi la tatu ambapo kati yao Tanzania Bara walikuwa watahiniwa 188,128 wakiwemo wasichana 84,509 na wavulana 103,619.

Akizungumza na Waandishi wa Habari Juni 11, 2023 jijini Dodoma, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Angelah Kairuki amesema zoezi hilo limezingatia takwimu za matokeo ya wanafunzi waliofanya mtihani wa kidato cha nne mwaka 2022 kutoka Tanzania Bara.

Amesema wanafunzi waliochaguliwa ni kutoka katika shule za serikali, binafsi, watahiniwa wa kujitegemea, waliofanya mtihani chini ya Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima na Vyuo vya Maendeleo ya Wananchi.


Post a Comment

Previous Post Next Post