SHIRIKA LA POSTA HUU NI WAKATI WENU WAKUJIPAMBANUA ZAIDI-DKT TULIA

 


Na,Saleh Lujuo-Dodoma.

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Tulia Ackson,amelitaka Shirika la Posta Tanzania kujipambanua kwa kuongeza nguvu zaidi ya kufanya kazi, kwakuwa sasa linaweshwa Kwa kiasi kikubwa na zoezi la anuani za makazi hivyo inakuwa rahisi kwao kufikisha huduma haraka Kwa wateja wao.

Dkt, Tulia,ametoa maagizo hayo  Leo Mei 18,2023 Jijini Dodoma  baada ya kutembelea mabanda ya Maonyesho katika viwanja vya Bunge yaliyoandaliwa na   wizara ya habari,mawasiliano na teknolojia ya habari  kuelekea uwasilishaji wa bajeti ya wizara hiyo hapo kesho.

Dkt,Tulia amesema kuwepo Kwa  mfumo wa anuani za makazi kunasaidia Kwa kiasi kikubwa Shirika hilo ,kuwafikia wateja endapo mteja atakuwa amesajili makazi yake hivyo kumuwezesha mtoa huduma wa Posta kufahamu Kwa haraka namba ya nyumba, jina la mtaa au Barabara, pindi anapopeleka mzigo Kwa mteja wake hivyo ni vyema kuongeza nguvu zaidi.

"Shirika letu la posta sasa nafikiri mjipambanue zaidi Kwa sababu mmewezeshwa Kwa kiasi kikubwa na zoezi la anuani ya makazi ukimutumia mtu barua  inaenda hadi nyumbani kwake kwakuwa tayari namba ya nyumba yake inafahamika  hivyo ongezeni nguvu''

Aidha Dkt Tulia amewataka wananchi ambao hawajasajili makazi yao kusajili Kwani mtu kujua anuani yake ya makazi zinasaidia kupata huduma Kwa haraka na kuchochea maendeleo.

 "Nimefurahi sana Leo nimeona zoezi hili la anuani za makazi ambayo yameanza mapema mwaka Jana na sasa tumefikia mahali ambapo yule aliyesajili anuani yake anaweza kuipata kiganjani Kwa kutumia aina yeyote Ile ya Simu kwahivyo nichukue fursa hii kuwapongeza wizara,.mtu kujua anuani yake ni muhimu sana na wale Wananchiwenzangu ambao hamujajisajili mjisajili muweze kupata huduma Kwa haraka" alisema Dkt Tulia 

Naye,Elia Madulesi ,Mkuu wa Mawasiliano na mambo ya Posta Kimataifa amesema, anuani za makazi zimewawezesha Kuwafikia wateja wao hadi majumbani hivyo kwao ni jambo kubwa sana ambapo linapunguza muda wa mwananchi kufikia ofisini.

 "Nimshukuru Rais kuweka msisitizo Kuwafikia wananchi Kwa huduma mbalimbali sisi Shirika la posta tunazo anuani za makazi ambazo mfumo wake upo tayari, tunazo huduma mbalimbali  katika kutoa huduma ikiwemo huduma ya vifurudhi   tunasema tunakufikiia popote ulipo sababu anuani Inatuwezesha kufika ulipo hivyo Mwananvhi  haitaji tena kututafuta sisi ndio tunakufuata popote pale ulipo" alisema Elia.

Post a Comment

Previous Post Next Post