Na,Saleh Lujuo -Dodoma.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge na Uratibu Mhe. Jenista Mhagama,ametaja mikoa sita inayolimwa bangi kwa wingi hapa nchini ikiwa ni pamoja na Arusha.
Mhe Mhagama ameyasema hayo mapema leo Mei 30 2023, Bungeni Dodoma wakati akitoa taarifa kwa vyombo vya habari kuhusu hali ya dawa za kulevya ya mwaka 2022 ambapo amessema kwa mujibu wa utafiti unaonyesha uwepo wa kiwango kikubwa cha uzalishwaji na ulimaji wa bangi nchini.
Waziri Mhagama amesema, kwa mwaka ujao wa fedha 2023/2024 Serikali imetenga bajeti ya shilingi Bilioni nane nukta saba (Bilioni 8.7) zitakazotumika kujenga vituo vya urekebu na ufundi stadi, vitakavyosaidia kubadilisha tabia za vijana wanaotumia dawa za kulevya,
“Vituo hivyo vitakuwa na kazi kubwa ya kuwaondoa kwenye matumizi ya dawa na kuwapa shunguli nyingine watakazotakiwa kuzifanya zitakazotokana na shughuli za ujuzi, ambazo watafundishwa kwenye vitu hivyo.” Amefafanua.
"kupitia Wizara ya Kilimo, Serikali itafanya utafiti, ili maeneo yanayolima bangi kibiashara kama vile Kisimiri Juu mkoani Arusha, kusaidiwa kulima mazao mbadala na juhudi za Serikali za kukomesha kilimo hicho zinaweza kuwasaidia kutoka kwenye biashara hiyo haramu kwa makusudi ya kuongeza kipato, na kuwafanya vijana na watumiaji kuwa salama".ameongeza.
Mikoa inayoongoza kwa kulima bangi nchini ni pamoja na Arusha, Manyara, Mara na Njombe,na baadhi ya Mikoa itakayojengwa vituo hivyo kuwa ni pamoja na Shinyanga, Kilimanjaro, Mwanza na Arusha.