TATHMINI YA BENKI YA DUNIA YA MWAKA 2022 INAONYESHA KUWA TANZANIA IMEPIGA HATUA KATIKA KUONGEZA USAWA WA KIJINSIA.

 

Na,Saleh Lujuo-Dodoma 

Makamu wa Rais,Dokta Philip Mpango,amezindua Mpango wa Jinsia wa  Anaweza unaofadhiliwa na Shirika la Kimataifa la Kifedha la Benki ya Dunia (IFC), kwa gharama ya zaidi ya Shilingi Bilioni 17.7.

Makamu wa Rais Dk.Philip Mpango amesema hadi kufikia Aprili mwaka huu serikali ilikuwa  imetoa sh.bilioni 30.9 kwa vikundi 5,120 vya wanawake katika Halmashauri 184 nchini.

Fedha hizo zimetolewa kwa lengo  kuboresha kipato na kuondoa umaskini kwa wanawake na wanaume pamoja kuhamasisha taasisi binafsi kutoa fursa kwa wanawake na kukukuza uchumi na kupunguza changamoto zilizopo katika ushiriki wa wanawake katika sekta binafsi hususan shughuli za ujasiriamali.

Akisoma hotuba ya Makamu wa Rais jijini Leo Mei 31,2023, Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Makundi Maalumu Dk.Dorothy Gwajima katika hafla ya uzinduzi wa program ya ANAWEZA iliyofadhiliwa na  Shirika la Kimataifa la Kifedha la Benki ya Dunia (IFC) alisema fedha hizo zimetolewa kupitia sheria ya fedha za mamlaka za serikali za mitaa.

“Kupitia sheria ya fedha za mamlaka za serikali za mitaa ya mwaka 2018 inayozitaka Halmashauri zote nchini kutenga asilimia 10 ya mapato yake ya ndani kwa ajili ya kutoa mikopo isiyo na riba kwa Makundi maalum ikiwemo wanawake asilimia nne, vijana asilimia nne na watu wenye ulemavu asilimia mbili.

Ameongeza kuwa:”Hadi kufikia April mwaka huu   sh.bilioni 30.9 zimekopeshwa kwa vikundi 5,120 vya wanawake katika halmashauri 184 nchini.

Dk.Gwajima alieleza kuwa kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Wanawake (WDF) unaosimamiwa na wizara anayoisimamia imetoa mikopo yenye thamani ya sh.milioni 664.5 kwa wanawake wajasiriamali 104 katika kipindi cha Julai 2022 hadi Aprili,mwaka huu.

Amesema Tanzania ni miongoni mwa  Mataifa yanayotekeleza malengo ya jukwaa la kimataifa ya kukuza usawa wa kijinsia ambapo Rais  Dk. Samia ni kinara wa utekelezaji wa Jukwaa hilo hususan kuhusu haki na usawa wa Kiuchumi.

Kwa mujibu wa Waziri huyo amesema Tanzania imetengeneza programu inayotekelezwa kwa ushirikiano wa Serikali na Sekta binafsi ili ifikiapo mwaka 2026 hali ya Wanawake iwe imebadilika kwa kiasi kikubwa.

“Programu hii inajumuisha kutengeneza mazingira bora ya malezi ya awali na uangalizi wa watoto katika ngazi ya jamii ikiwemo masokoni lakini pia katika maofisi ili kuhakikisha huduma za msingi kama vile maji na umeme zinafika kwa ukamilifu vijijini ili kutatua changamoto zinazowakumba wanawake,”ameeleza

Amefafanua kuwa Programu ya ANAWEZA itachangia kufanikisha utekelezaji programu wa kizazi chenye usawa hapa nchini na kuwezesha wanawake kushiriki katika nafasi mbalimbali za uongozi.

“Ni matarajio yangu kuwa mpango utashirikisha sekta binafsi hapa nchini ili kukuza upatikanaji wa fursa za wanawake katika nafasi za uongozi na ajira bora ili kuchochea ukuaji wa uchumi nchini.

Ameongeza kuwa :”Utafiti unaonyesha kuwa kuziba pengo la kijinsia kati ya ajira za wanaume na wanawake kunaweza kuongeza Pato la Taifa la muda mrefu kwa kila mtu kwa asilimia 4.8.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa IFC wa Afrika Mashariki Jumoke Dokunmu amesema asilimia 34 ya wanawake wameajiriwa nchini ambapo amesema kuwa program ya ANAWEZA itatekelezwa kwa miaka mitano na inalenga kushughulikia changamoto zilizopo ili kuwezesha ushiriki wa wanawake katika sekta binafsi,  nafasi za uongozi na ujasiriamali wenye ufanisi endelevu.

Amesema programu hiyo itakagharimu fedha za Kimarekani milioni 7.5, inaendana na Dira ya Maendeleo ya Taifa ya mwaka 2025, Mpango wa Taifa wa Maendeleo wa Miaka Mitano.

“Wanawake wanaweza kuwa injini ya ukuaji wa uchumi wa Tanzania, hivyo kuwawezesha wanawake kunachukua jukumu kubwa la kukuza uchumi na kuwezesha upatikanaji wa maisha bora kwa watu binafsi na familia zao” amesema.

Ameeleza kuwa kwa mujibu wa tathmini ya Benki ya Dunia ya mwaka 2022 kuhusu hali ya jinsia Tanzania inaonyesha kuwa Tanzania imepiga hatua katika kuongeza usawa wa kijinsia kwa kufanya jitihada za kukabiliana na ukosefu wa usawa wa kijinsia katika Nyanja zote za maisha ya wanawake.

Naye Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Zanzibar, Riziki Pembe amesema kuwa Rais wa Zanzibar Dk. Husein Ally Mwinyi anathamini kazi zinazofantwa na wanawake ambapo amekuwa akiwateu kushika nafasi mbalimbali za uongozi.

Mpango huo unatekelezwa kwa kipindi cha miaka mitano na umebuniwa na IFC kwa kushirikiana na watanzania" amesema Dokunmu.

Post a Comment

Previous Post Next Post