Na,Saleh Lujuo-Dodoma
Ukosefu wa taulo za kike kwa wanawake hususani wasichana mashuleni mara nyingi husababisha kukosa kuhudhuria masomo kila mwezi wanapokuwa hedhini ambapo jamii na Taasisi za umma zimeshauriwa kuwasaidia wanawake kwa kutoa msaada wa taulo za kike.
Promota wa Lady In Red Mbunge wa Viti Maalum Sophia Mwakagenda ametoa kauli hiyo Jijini Dodoma wakati akizungumza mbele ya wabunge waliopigana katika pambano lililofanyika Mwezi mmoja uliopita Jijini Dodoma kutokana na pambano hilo kuchangia Taulo za Kike elfu 23000.
"watu wenye uwezo changieni hizi taulo za kike kwa wanawake,na wasaidieni watu wenye saratani na watoto wa kike, ili kuwapa mahitaji mbalimbali zikiwemo taulo za kike" amesisitiza.
Aidha Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Kigoma Sylvia Sigula amesema yeye kama mwakilishi wa wananchi anapenda kutumia jina lake kiwasaidia wanawake kwani nafasi aliyonayo kama Mbunge ni kuwatumikia wananchi ambapo amekiri kwamba alipambana katika pambano mwezi uliopita kutokana na ajenda ya kuwasaidia wasichana pamoja na wanawake.
Hata hivyo Mbunge wa Viti Maalum (CHADEMA)Mhe.Salome Makamba ametoa wito kwa watu wenye Majina makubwa kutumia majina yao katika kuisaidia jamii.
"Tujitoe ndugu zangu kuwasaidia wanawake wenye mahitaji mbalimbali, uwezo ulionao jitokeze na uwasaidie" amesema makamba.
Hafla hiyo imeambatana na utoaji Tuzo kwa washiriki waliopigana katika pambano hilo kwa lengo la kuzihamasisha Taasisi mbalimbali nchini kuwasaidia wanawake taulo za kike hususani wasichana mashuleni