WAZEE WA YANGA DODOMA WAMTAKA KARIA KUOMBA RADHI

WAZEE WA YANGA DODOMA WAMTAKA KARIA KUOMBA RADHI


Na,Saleh Lujuo-Dodoma

Wazee wa timu ya mpira wa Miguu Young Africans  Mkoa wa Dodoma wamekemea vikali kauli ya Rais wa shirikisho la mpira wa miguu Tanzania Wallace Karia na kumtaka Rais huyo kuomba radhi kufuatia kauli aliyoitoa kuhusu timu hiyo.

kauli hiyo ya wazee wa Yanga imekuja mara baada ya kuahirishwa Kwa dabi ya karikakoo na Kutokana na kauli aliyoitoa Rais karia ambayo wameita kauli ya kuwafokea.

Akizungumza  leo Machi 18,2025 jijini Dodoma mbele ya Waandishi wa habari kwa niaba ya wazee wengine Mzee Abdalah Mtosa amesema hawaoni sababu ya kurudia mchezo kwa sababu mchezo huo ulipangwa kisheria na kuahirishwa bila utaratibu siku ya Machi 8,2025.

Mzee Mtosa amesema alichukizwa sana kuahirishwa kwa mchezo wa machi 8 mwaka huu ambapo amesema hawana imani na Karia kwa sababu hana mapenzi ya dhati na Yanga.

"Nimepokea kwa masikitiko makubwa sana Kwa kuahirishwa kwa mchezo wa Machi 8 mwaka huu, kwahiyo na sisi hatuna imani na karia kwani tunajua wazi hana mapenzi ya dhati na yanga." Amesma

"hakuna haja tena ya mechi kufanyika kwa wakati mwingine,haina Maana" Amesema Mtosa

Mzee Bodar Awadhi  ambaye naye ni mzee wa Yanga amesema kuahirishwa kwa mechi kumewafanya mashabiki wa soka nchini kutokuwa na imani na viongozi na mashabiki wengi hawaitaki tena hiyo mechi.

"Msimamo wetu kama wazee wa Yanga ni kutokurudia mechi na huyo Rais wa TFF ametudhalilisha wanayanga na kama ameshindwa mpira awachie wengine wafanye". Amesema.

Kwa upande wake Mratibu wa yanga Mkoa wa Dodoma Elisha Ngwando amesema kauli aliyoongea karia hawaikubaliani nayo kwani soka huendeshwa kwa taratibu, Sheria, kanuni na miongozo.


Post a Comment

Previous Post Next Post