TUTAHAKIKISHA MAONO YA RAIS SAMIA SULUHU HASSAN YANATIMIA KWA MAGEREZA YOTE NCHINI KUACHANA NA MATUMIZI YA KUNI NA KUTUMIA NISHATI SAFI YA KUPIKIA-CGP YORAM






TUTAHAKIKISHA MAONO YA RAIS SAMIA SULUHU HASSAN YANATIMIA KWA MAGEREZA YOTE NCHINI KUACHANA NA MATUMIZI YA KUNI NA KUTUMIA NISHATI SAFI YA KUPIKIA-CGP YORAM

Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza Nchini (CGP) Jeremiah Yoram Katungu leo Octoba 16,2024 ametembelea mradi wa nishati safi ya kupikia Gereza Kuu Butimba na kusifu uongozi wa Magereza Mkoa wa Mwanza kwa kuhakikisha maono ya Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan yanatimia kwa Magereza yote nchini kuachana na matumizi ya kuni na kutumia nishati safi ya kupikia.

CGP Katungu, amesema hayo wakati akizungumza na maafisa na askari wa Magereza Mkoa wa Mwanza katika kikao alichokiitisha mara baada ya kukagua miradi inayofanywa katika Mkoa huo.

Katika kikao hicho, CGP Katungu alisisitiza umuhimu wa kusimamia vizuri miradi hii ili kusaidia kutatua changamoto ndogo ndogo zinazotokea katika vituo husika. Aliongeza kuwa katika ukusanyaji wa maduhuli kwa mwaka huu, lengo ni kukusanya milioni 800. Alipongeza watendaji wake kwa mafanikio ya kukusanya zaidi ya malengo yaliyowekwa, akitolea mfano wa kukusanya milioni 260 badala ya milioni 200 zilizopangwa katika kota ya kwanza ya mwaka.

“Katika miradi hii ndiyo maduhuli ya serikali yanapatikana, hivyo wakuu wa Magereza mikoa mkishirikiana na wakuu wa Magereza kupitia mabaraza yenu, hakikisheni mnawatangazia maafisa na askari idadi ya miradi pamoja na mapato na matumizi,” alisisitiza CGP Katungu.

Akijibu hoja mbalimbali zilizowasilishwa na maafisa na askari, CGP Katungu alieleza kuwa Jeshi linaendelea kufuatilia ili kuzipatia ufumbuzi, huku akiwataka kuongeza ushirikiano baina ya maafisa na askari.


Post a Comment

Previous Post Next Post