MKUTANO WA JUKWAA LA TASNIA YA KUKU NA NDEGE WAFUGWAO KWA NCHI WANACHAMA SADC KUFANYIKA TANZANIA KWA MARA YA KWANZA.


MKUTANO WA JUKWAA LA TASNIA YA KUKU NA NDEGE WAFUGWAO KWA NCHI WANACHAMA SADC KUFANYIKA TANZANIA KWA MARA YA KWANZA.

Na,Saleh Lujuo-Dodoma

Kutokana na serikali kuendelea kuwahimiza vijana na wanawake kuchangamkia fursa za uwekezaji zilizopo katika tasnia ya kuku na ndege wafugwao,imewahimiza kushirika katika jukwaa la tasnia ya kuku na ndege wafugwao kwa nchi wanachama kusini mwa Afrika SADC utakao fanyika hapa nchini.

Mkutano huo wa jukwaa la tasnia ya kuku na ndege wafugwao Kwa nchi za SADC utahudhuriwa na wadau zaidi ya 2000 na waoneshaji 50 wa bidhaa kutoka ndani na nje ya nchi watashiriki.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Oktoba 11,2024 jijini Dodoma Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi Prof. Riziki Shemdoe amesema mkutano huo utafanyika tarehe 16 na 17 Oktoba mwaka huu katika hoteli ya Serena jijini Dar es salaam na kufuatiwa na maonesho ya Kitaifa ya Tasnia ya Kuku na ndege wafugwao Oktoba 18 na 19 katika  ukumbi wa Mlimani City huku  mgeni rasmi anatarajiwa kuwa  Naibu Waziri Mkuu Dkt.Doto Biteko. 

Prof.Shemdoe amesema kuwa mkutano huo umelenga kujadili kubadilishana uzoefu Kutoka nchi za SADC pamoja na kubainisha fursa za kimkakati zinazohusu tasnia ya kuku na ndege wafugwao zilizopo katika nchi za SADC pamoja na  kuweka maazimio yatakayoifanya tasnia hiyo iweze kuwa shindani.

"Mkutano huu unalenga kuongeza fursa za masoko ndani na nje ya nchi za SADC kuongeza ajira, kuinua mchango wa tasnia katika pato la taifa na kuchangia katika usalama na lishe". Amesema

Aidha, amesema mkutano huo utatoa nafasi kwa Tanzania kuonesha fursa za uwekezaji zilizopo katika tasnia ya kuku na ndege wafugwao pamoja na kuongea wigo wa masoko ya kuku na bidhaa zake katika nchi za SADC.

"Pia utaongeza ushiriki wa vijana na wanawake na kuimarisha ushirikiano baina ya Tanzania na nchi za SADC katika Tasnia ya Kuku". Ameongeza

Samabamba na hayo amesema Tasnia ya Kuku na ndege wafugwao ni muhimu Kwa ustawi wa uchumi ambapo Asilimia 55 ya kaya hapa nchini Tanzania zinafanya shughuli za ufugaji kuku.

"Maonesha ya tasnia ya kuku na ndege wafugwao ni bure,hivyo wizara inatoa rai Kwa wananchi wote hususani wafanyabiashara ya kuku na ndege wafugwao katika mnyororo wa thamani kushiriki maonesho hayo". Amesisitiza 

Tanzania Kwa mara ya kwanza imepata fursa ya kuwa mwenyeji wa mkutano wa jukwaa la Tasnia ya Kuku na ndege wafugwao kwa nchi wanachama wa jumuiya ya maendeleo kusini mwa Africa (SADC) na utafuatiwa na maonesho ya Kitaifa ya Tasnia ya Kuku na ndege wafugwao.

Post a Comment

Previous Post Next Post