SEPESHA RUSHWA MARATHON 2024 YABEBA AJENDA ISEMAYO #ACHARUSHWA YA NGONO.
Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mjiini Mh Jabir Shekimweri amsema kuwa anafurahishwa na Taasisi isiyo ya Kiserikali ya"Anti Corruption Voices "ya Jijini Dodoma namna ambavyo inafanya kazi ya kueleimisha jamii kuepuka vitendo vya rushwa na kuongeza kuwa mapambano ya rushwa yanapaswa kuwa endelevu.
Mh Shekimweri ameyaeleza haya leo Oktoba 7,2024 Jijini hapa kwenye Mkutano na Wanahabari juu ya kuanza kwa msimu wa mbio za Sepesha Rushwa Marathon 2024 ambazo zitafanyika hapa Jijini Dodoma Desemba 1,2024.
Awali akizungumza Mwenyekiti wa Bodi ya kampeni ya Sepesha Rushwa Dkt. Dina Daniel wa Taasisi hiyo isiyo ya kiserikali ya Sauti ya wapinga rushwa "Anti Corruption Voices" ya Jijini hapa amesema licha ya juhudi zinazofanywa na Serikali kuipinga rushwa lakini bado kuna haja ya kuendelea kuelimisha Jamii namna ya kuepukana na rushwa ya ngono.
Taasisi hiyo ambayo imebeba ajenda ya kupinga vitendo vya rushwa kwenye jamii imesema rushwa si sehemu ya utamaduni wa mtanzania na hivyo Jamii nzima inapaswa kuikataa kwa vitendo kwani inadhalilisha utu wa mtu.
Aidha Mwenyekiti huyo ameeleza kuwa Rushwa ya ngono bado inanuka huku akitolea mfano kuwa kuna baadhi ya wafanyakazi wakiwa kwenye siku za wanakatwa mshahara siku zote wanazokaa nyumbani.
"Rushwa ni adui wa haki inadhalilisha utu wa mtu, imefikia hatua baadhi ya wanawake wanapokuwa kwenye siku zao wanakata mshahara kufidia zile siku ambazo walishindwa kumudu kutokana na maumivu, adhabu hii ni unyanyasaji na tunaiita rushwa,"
Kuhusu kuanza kwa msimu wa mbio za marathoni zilizopewa jina la "Sepesha Rushwa" na kupewa kauli mbiu ya "Acha Rushwa ya Ngono" zinaenda kumaliza rushwa kwenye jamii na kueleza kuwa kwa awamu hii nguvu inaelelezwa kwa vijana ambapo itawaelimisha namna ya kuondokana na rushwa ya ngono na kuepukana na rushwa hiyo
"Rushwa imekuwa ni tatizo kwenye jamii, Mwalimu nyerere aliliona tangu Zaman akasema rushwa ni adui wa haki,tuitangazie dunai kuwa rushwa inakosesha uhalali wa huduma na kufifisha ndoto za watu,kuna haja ya kuelimishana na kukumbushana namna ya kuwajibika,"
kwa upande wake Mwakilishi kutoka Mamlaka ya Kuzuia na kupambana na Rushwa TAKUKURU Mkoa wa Dodoma Hazina Eugene amesema wamekuwa wakishirikiana na jamii katika kuhakikisha wanapiga vita adui mkubwa rushwa ambapo kwa miaka ya hivi karibuni wameweza kushughulikia kesi mbalimbali.
" Rushwa ni adui wa haki hivyo ni vyema jamii kutambua na kuacha kutoa na kupokea rushwa ya aina yeyote, " Amesema Mwakilishi huyo wa TAKUKURU
Pamoja na Mambo mengine Kampeni hiyo itatumia miezi miwili kuelimisha jamii kuanzia Oktoba hadi Desemba ambapo jumla ya Washiriki 5000 watahudhuria lengo likiwa ni kusambaza elimu ya rushwa ya ngono na kuwa sehemu ya mabalozi kwa jamii kwa ujumla.