TUMIENI TEKNOLOJIA ZA KISASA KATIKA KILIMO ILI MZALISHE KWA TIJA-SILINDE







TUMIENI TEKNOLOJIA ZA KISASA KATIKA KILIMO ILI MZALISHE KWA TIJA-SILINDE

Na,Saleh Lujuo-Dodoma

Serikali kupitia Wizara ya Kilimo imedhamiria kuwawezesha vijana katika sekta ya kilimo kwa kuwapatia dhana mablimbali ikiwemo matrekta ili wakulima waweze kulima kwa tija huku ikiwataka wananchi kujitokeza katika maonyesho ya  nanenane kujionea teknolojia za kisasa ambazo zitawasaidia.

Kauli hiyo ya serikali ameitoa Naibu Waziri wa kilimo,David Silinde  katika viwanja vya nanenane  Jijini  Dodoma mara baada ya kutembelea mabanda mbalimbali na kujionea teknolojia za kilimo.

"Kama serikali tumejipanga katika kuhakikisha vijana wanapata uelewa kuhusu kilimo na tayari tushatoa maelekezo kwa Mikoa na Halmashauri zote nchini kutenga maeneo kwajili ya vijana ili Taifa letu la Tanzania lijitosheleze na mazao ya kilimo". Amesema Silinde

kwa upande wake Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya Kampuni ya PASS Leasing Co.Ltd, Rosebud Kurwijila amesema kampuni hiyo imekabidhi vifaa vya kulimia kwa wakulima  zikiwemo  trekta 9 zenye  thamani millioni  401.76 kwa wakulima wa mkoa wa Dodoma,wilaya ya Kongwa na Chemba.

"Uwezeshaji huu tunategemea utakwenda kuongeza uzalishaji kwa kulima mashamba zaidi ya ekari 2000; kutengeneza ajira za moja kwa moja zisizopungua 30 na kuwafikia wanufaika  takribani 300 kwa kipindi cha msimu mmoja". Amesema 

"Katika kanda ya kati, mkoa wa Dodoma na Singida tumeshawezesha zana zenye jumla ya thamani ya takribani ya bilioni 13 kwa wajasiliamali zaidi ya 350 kati yao vijana ni 25%". Ameongeza

Jalia Abdalah Rashid ambaye ni mkulima kutoka wilaya ya Kongwa ameishukuru kampuni ya PASS  kwa kuweza kuwaletea zana za kilimo za kisasa kwani anaamini kulima kwa kutumia trekta kutampa uwezo wa kulima ekari nyingi kwa muda mfupi na kufikia malengo aliyokuwa akiyatamani kwa muda mrefu.

"Nanawashauri wakulima wenzangu kuacha kulima kizamani na wanatakiwa kuhamia kwenye kilimo cha kisasa na chenye tija". Amewasisitiza wakulima.

Maonesho ya 31 ya sherehe za nanenane kitaifa kwa mwaka huu 2024 yanafanyika Jijini Dodoma yakiongozwa na kauli mbiu isemayo; chagua viongozi Bora wa serikali za mitaa kwa Maendeleo Endelevu ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi".


Post a Comment

Previous Post Next Post