MOI IMEDHAMIRIA KUSOGEZA HUDUMA ZA KIBINGWA KWA WANANCHI WOTE


MOI IMEDHAMIRIA KUSOGEZA HUDUMA ZA KIBINGWA KWA WANANCHI WOTE 

Na,Saleh Lujuo-Dodoma

Licha ya serikali kuemdele kuwahimiza wananchi kufanya mazoezi na kupima Afya zao mara Kwa mara,Taasisi ya mifupa na ubongo Muhimbili (MOI) imesema imesogeza huduma za kibigwa kwa wananchi ambapo wamepokea wagonjwa mbalimbali wenye matatizo ya mifupa, mgongo, kichwa, mishipa ya fahamu, wenye matatizo ya lishe lakini pia utaalamu wa mahitaji ya mazoezi tiba.

Dkt. Consolata Shayo Daktari wa ubongo, mgongo na mishipa ya fahamu kutoka kwenye taasisi hiyo Ameyasema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari katika viwanja vya maonesho ya 88 nzuguni Dodoma kuhusu mwitikio wa wanachi kupewa huduma mbalimbali zinazotokana na taasisi hiyo.

Aidha amesema kuwa wanatoa huduma ya viungo saidizi pia utaalamu wa ultrasound ambapo huduma zote hizo ni bure ambapo mwitikio wa wananchi ni mkubwa na wanaendelea kujitokeza kwa wingi.

"Kiukweli mwitikio wa wananchi ni mkubwa na tumekuwa tukipokea wananchi kutoka sehemu mbalimbali ndani na nje ya Dodoma na tumekuwa tukiwapatia matibabu haya buree na wengi wamekuwa wakifurahia huduma zetu na sisi kama taasisi tunafurahia kuwahudumia watanzania wenzetu"Amesema

Sambamba na hayo amewashauri watanzania ambao bado hawajafika kwenye banda lao wahakikishe wanafika ili waweze kuwasaidia kiufanisi zaidi na kwasababu wamewasigezea huduma hizo basi wafike na kwa wale ambao wanahitaji matibabu zaidi wanawaandikia Rufaa ili waweze kwenda Hospitali kubwa na wengine wamekuwa wakiwaandikia dawa.

"Pia wale wenye matatizo ya uchakavu wa migongo, mifupa na magoti wengi wanakuja kwasababu wana shida hiyo kutokana na umri lakini pia kutokana na aina ya maisha ambayo wameishi hapo awali na ambayo wanaendelea kuyaishi sasaivi,kwani kazi zetu tunazozifanya tunakaa mda mrefu bila kifanya mazoezi"Amesisitiza

Kadhalika, ameongeza kuwa baadhi ya watu hupata maradhi kutokana na lishe duni hivyo ni rahisi mifupa kuchakaa kwa urahisi,hivyo wanapokuja wanakuwa na matatizo makubwa sana ya mgongo,magoti pamoja na miguu na kazi yetu ni kuwapa ushauri wa kibigwa na wengi wakitoka hapa wanakuwa wameridhika na tunaamini wataendelea vizuri na afya wanavyoenda majumbani na katika shughuli zao.

Amesema wananchi wengi wanaofika tangu waanze kutoa huduma wanakuwa wanaumwa sanasana magoti pamoja na lishe duni na wengine kuwa na uzito mdogo kuliko urefu wao hivyo tumekuwa tukitoa huduma hizo zaidi haswa.

Sanjari na hayo amemalizia kwa kutoa wito kwa wananchi kubadilisha miundo ya lishe pamoja na jinsi tunavyoishi kwani wengi wanaokwenda niwafanyakazi wa maofisini wanaokaa zaidi ya masaa matatu manne hajasimama wala kunyoosha mgongo wake,hata kutembea tu kufanya zoezi fupi hivyo wanawashauri kuto kukaa zaidi ya dakika 45 hadi lisaa bila kunyoosha miguu na mgongo.

"Tunaendelea kutoa ushauri kwa siku wajitahidi watembee walau hatua elfu 10 kwa siku tusizoee kupanda panda lifti tupande ngazi kwa wale ambao wanakosa muda wa kufanya mazoezi lakini wengi ni wale wanaochelewa kula wanakula saa 4 usiku alafu unakuta kala ugali mboga ya majani kidogo na nyama nyingi jambo ambalo siyo zuri kiafya"

Post a Comment

Previous Post Next Post