WAUGUZI NA WAKUNGA WALIOTAHINIWA WAMETAKIWA KURIPOTI KWENYE VITUO VYA MTIHANI NA ATAKAYEKOSA KUFIKA ATAJIKOSESHA KUFANYA MTIHANI-BI. HAPPY MASENGA
Na,Saleh Lujuo-Dodoma
Kaimu Msajili Baraza la uuguzi na ukunga Tanzania Bi. Happy Masenga amewataka watahiniwa wote waliojisajili kwa ajili ya mtihani wa usajili na leseni kufika katika vituo walivyoomba siku ya kesho Disemba 28,ili kupata maelekezo na namba za mtihani.
Mtihani huo unatarajiwa kufanyika Disemba 29,2023 katika vituo mbalimbali vilivyo tambuliwa na kukubalika na baraza katika mikoa mbalimbali hapa Nchini.
Bi.Masenga ambaye ni Kaimu Msajili wa Baraza hilo ametoa msisitizo huo Leo Disemba 27,2023 Jijini Dodoma ambapo amesema atakayekosa kufika atakuwa amejikosesha nafasi ya kufanya mtihani huo.
"Mtihani huo utafanyika katika vituo vilivyotambuliwa na kukubalika na baraza katika mikoa mbalimbali hapa nchini kuwa ni Mwanza kwenye kituo cha Taasisi ya afya na sayansi shirikishi (TANDABUI)ambapo idadi ya watahiniwa watakaofanya mtihani ni 991,Dar Es Salaam-Chuo Kikuyu cha Kampala watahiniwa 972 na Dodoma -Chuo Kikuyu cha St. John's watahiniwa 450 na Chuo cha elimu ya Biashara (CBE) 350". Amesema Bi.Masenga
"Vituo vingine ni Kilimanjaro-Chuo cha Stephan Moshi watahiniwa 477,Mbeya-Chuo cha Afya na Sayansi shirikishi Mbalizi 569,Iringa-Chuo kikuu cha Katoriki Ruaha watahiniwa 191 na Tabora 166". Ameongeza
katika hatua nyingine Bi.Masenga ametumia nafasi hiyo kutoa wito kwa wauguzi na wakunga waliopo kazini kuzingatia maadili na kiapo cha taaluma ya uuguzi na ukunga.
"Natoa rai kwa wote wauguzi na wakunga kufuata maadili na kiapo Cha taaluma ya uuguzi na ukunga, tunayomiongizo inayotuelekeza kuhusu maadili pitieni na mfanye kazi kwa kuzingatia maadili kwa sababu Umma unatutarajia sisi wakunga na wauguzi". Amesisitiza
Jumla ya watahiniwa 4166 wamekidhi sifa za kufanya mtihani huo wakiwemo 3917 ambao wanafanya mtihani kwa mara ya kwanza,na 248 wanaorudia.
Tags:
Habari