WAJASIRIAMALI MILIONI 8.6 WAMENUFAIKA NA MIKOPO KUPITIA BARAZA LA TAIFA LA UWEZESHAJI WANANCHI KIUCHIMI.

WAJASIRIAMALI MILIONI 8.6 WAMENUFAIKA NA MIKOPO KUPITIA BARAZA LA TAIFA LA UWEZESHAJI WANANCHI KIUCHIMI.

Na,Saleh Lujuo-Dodoma.

Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC,katika kipindi cha Mwaka 2022/2023,imefanikiwa kutoa mikopo yenye thamani ya Shilingi Trilioni 6.1 kwa wajasiriamali Milioni 8.6 kupitia mifuko inayoiratibu.

Aidha, hadi kufikia Juni 2023 ajira 145,245 zimezalishwa kwa watanzania kwenye miradi ya kimkakati na uwekezaji.

Katibu Mtendaji wa baraza la taifa la uwezeshaji wananchi kiuchumi (NEEC) Bi.Being'i Issa  ameyasema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma kuhusu utekelezaji wa vipaumbele vya baraza hilo kwa mwaka wa fedha 2023/2024.

Aidha amesema kuwa jumla ya makampuni ya Kitanzania 2, 010 yamenufaika kwa kupata kazi mbalimbali katika miradi inayosimamiwa na kuratibiwa na Baraza.

"lengo kubwa ni kutoa fursa kwa watanzania  kuanzisha na kuendeleza viwanda vidogo na vya kati, kupata mikopo yenye riba nafuu hususan kwa viwanda vinavyochakata mazao ya kilimo na mifugo" amesema.

Aidha ameongeza kuwa hadi Juni 2023  mikopo yenye thamani ya Shilingi bilioni 3.8 ilitolewa kwa miradi 65 katika mikoa 13 ikiwa ni nia ya Serikali ya kuhakikisha huduma za kuwawezesha wananchi kiuchumi zinapatikana karibu na wananchi".amesema.

"hadi Machi, 2023 jumla ya vituo vya uwezeshaji 18 vimeanzishwa katika mikoa 6 ya Shinyanga (Vituo 2), Geita, Singida, Rukwa (Sumbawanga), Kigoma (Vituo 6) na Dodoma (Vituo 7), ambapo vituo viwili (Morogoro na Pwani) viko kwenye hatua za kuongeza huduma wezeshi na kuweza kuwa vituo vya uwezeshaji kamili kwa mwaka wa fedha 2022/2023 vituo vya uwezeshaji vimetoa mikopo yenye thamani ya Shilingi bilioni 9.4 kwa wajasiriamali 4,017nchini".amesisitiza.

Kwa mwaka wa fedha 2022/2023 vituo vya uwezeshaji vimetoa mikopo yenye thamani ya Shilingi bilioni 9.4 kwa wajasiriamali 4,017nchini.

" imeanzishwa kanzi data ya Taifa ya uwezeshaji ambayo lengo kuu ni kuwaunganisha wawekezaji na watoa huduma mbalimbali za biashara. Hadi kufikia mwezi Juni 2023 jumla ya watoa huduma 186 na Wawekezaji 17 walikuwa wamesajiliwa"

Kwa upande wake Msemaji Mkuu wa Serikali Gerson Msigwa amewataka watanzania kujiepusha na mikopo inayoumiza na utapeli unaofanyika mitandaoni kuhusiana na mikopo hiyo.

Baraza la Taifa la Uwezeshaji wananchi Kiuchumi lilianzishwa mwaka 2004 likiwa na majukumu mbalimbali ikiweko kusimamia,kuratibu,kufuatilia na kutathimini utekelezaji wa shughuli za uwezeshaji uchumi Tanzania Bara.

Post a Comment

Previous Post Next Post