TEHAMA NI NJIA BORA YA KUTUNZA TAARIFA ZA AFYA NCHINI-DKT. SHEKALAGHE


TEHAMA NI NJIA BORA YA KUTUNZA TAARIFA ZA AFYA NCHINI-DKT. SHEKALAGHE

Na,Saleh Lujuo-Dodoma.

Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt.Seif Shekalaghe amesema Serikali inatumia Fedha nyingi sana Kwenye kutumia makaratasi katika kuchukua taarifa za Afya nchini ambapo amemwagiza Mkurugenzi wa TEHAMA wizara hiyo kufanya mchakato wa haraka kuhakikisha mifumo yote ya afya iwe inasomana kwa wakati mmoja ili kuweza kuboresha huduma za afya.

Dkt.Shekalaghe ametoa kauli hiyo leo Jijini Dodoma katika uzinduzi wa Kituo cha Umahiri kuhusu masuala ya afya ya Kidigitali -CDH ambapo amesema kupitia kituo hicho huduma za afya zinaimarika kwani taarifa zote za afya kutoka hospitali zote zitaweza kusomana kwa wakati mmoja.

“Taarifa zinatakiwa kamilifu ili kila mhusika aweze kuona kwa wakati, sio kiongozi yeyote anataka kuuliza kuna madaktari bingwa wangapi sihitaji kukupigia simu ninachotakiwa ni kuingia tu kwenye mfumo na kupata taarifa updated( za wakati huohuo)”amesema .

Aidha,Dkt.Shekalaghe amesema Kila Mhudumu wa Afya ngazi ya Jamii ataingizwa kwenye mfumo ambapo mfumo huo ni moja ya maagizo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt.Samia Suluhu Hassan ya kuhakikisha mifumo yote inasomana.

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa TEHAMA Wizara ya Afya Silvanus Ilomo amesema kituo hicho sio kwa ajili ya Wizara ya Afya pekee hivyo mlango uko wazi hata Wizara zingine kukitumia kituo hicho.

Naye Mwakilishi wa Mamlaka ya Serikali Mtandao(eGa )Sultana Seif amesema mamlaka hiyo itaendelea kushirikiana na Wizara ya Afya kuhakikisha mifumo inakuwa salama .

Mkurugenzi mkaazi wa Taasisi isiyo ya kiserikali ya PATH amesema Taasisi hiyo imejiwekea mikakati ya kuongeza ufanisi katika utoaji huduma ya Afya kwa kuiweka Mifumo ya TEHAMA katika ngazi ya huduma ya Afya ya Msingi ili Wananchi waweze kupata huduma bora za afya.

Post a Comment

Previous Post Next Post