VIJANA 3,258 WAMEPATA FURSA YA KUJIFUNZA NA KUENDELEZA UJUZI WAO KATIKA VYUO VYA VETA DODOMA,MANYARA, LINDI NA KIPAWA

VIJANA 3,258 WAMEPATA FURSA YA KUJIFUNZA NA KUENDELEZA UJUZI WAO KATIKA VYUO VYA VETA DODOMA,MANYARA, LINDI NA KIPAWA

Na,Saleh Lujuo-Dodoma 

Serikali imesema Vijana ni rasilimali muhimu na nguvu kazi yenye kuleta mabadiliko na kuchangia katika maendeleo ya nchi ambapo imetoa wito kwa Wabia wa Maendeleo, na sekta binafsi kuendelea kuunga mkono juhudi za Serikali kwa ajili ya kukuza ujuzi na ajira kwa vijana. 

wito huo umetolewa leo Jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Kilimo Mhe. Anthony Mavunde katika kongamano la ujuzi na Ajira ambapo amezitaka sekta binafsi kuwawezeshe vijana kutimiza ndoto zao, kuendeleza ujuzi wao ili wachangie  katika ujenzi wa Tanzania bora na endelevu.

"Tunahitaji kuwekeza katika miundombinu bora ya elimu na mafunzo, kuboresha upatikanaji wa mitaji na mikopo kwa vijana wajasiriamali, na kuweka mazingira rafiki ya biashara". amesema 

"Pia,tuendelee kuhamasisha ushirikiano kati ya vyuo vya ufundi, taasisi za elimu na waajiri ili kuhakikisha kuwa mafunzo yanalingana na mahitaji halisi ya soko la ajira". ameongeza.

Aidha, Waziri Mavunde amewahimiza wahitimu wa  Mradi wa kukuza ajira kwa vijana (E4DT  kuwa na ujasiri na kujiamini katika kutumia ujuzi wao na kuanzisha miradi yao wenyewe.  

"uaminifu, uadilifu na bidii katika kazi ni vigezo muhimu sana katika mafanikio kwenye ajira ya kuajiriwa au kujiajiri". amesisitiza.

"nendeni mkatumia ujuzi wenu vizuri na mkawe mabalozi wa mafunzo ya ufundi stadi yanayotolewa kwenbye Vyuo vya VETA nchini". ameongeza.

Sambamba na hayo, Mradi wa kukuza ajira kwa vijana nchini Tanzania (E4DT), umedhamiria kuwafikia vijana zaidi ya 4000 ambapo hadi sasa, tayari vijana 3,258 wamepata fursa ya kujifunza na kuendeleza ujuzi wao katika vyuo vya VETA Dodoma, Manyara, Lindi, na Kipawa.

Kwa upande wake CPA Anthony Kasore, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa VETA ameishukuru serikali Kwa kuendelea kuwekeza katika miundombinu bora ya elimu na mafunzo pamoja na kuboresha upatikanaji wa mitaji na mikopo kwa vijana wajasiriamali, na kuweka mazingira rafiki ya biashara.

Mradi wa kukuza ajira kwa vijana nchini Tanzania (E4DT), umefadhiliwa na Shirikisho la Ujerumani la Ushirikiano wa Kiuchumi na Maendeleo (BMZ), Shirika la Ushirikiano wa Maendeleo la Norway (Norad), Umoja wa Ulaya (EU), na Shirika la Ushirikiano wa Maendeleo la Korea (KOICA) akiwa ni mfadhili mkuu

Post a Comment

Previous Post Next Post