TUME YA TEHAMA HADI SASA IMESHASAJILI WATAALAM WA TEHAMA 1,600 WANAOHUDUMIA NCHI NZIMA-DKT. MWASAGA

TUME YA TEHAMA HADI SASA IMESHASAJILI WATAALAM WA TEHAMA 1,600 WANAOHUDUMIA NCHI NZIMA-DKT. MWASAGA

Na,Saleh Lujuo-Dodoma.

Tanzania imetajwa kuwa ni nchi ya pili kwa Afrika duniani kwa usalama katika uchumi wa kidijitali hali inayovutia kampuni nyingi za TEHAMA kuja  kuwekeza Tanzania.

Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya TEHAMA (ICTC),Dokta Nkundwe Mwasaga amebainisha hayo Jijini Dodoma wakati akieleza utekelezaji wa majukumu na mwelekeo wa Tume hiyo kwa mwaka 2023/2024 ambapo hadi sasa TUME imeshasajili wataalam wa TEHAMA 1,600 wanaohudumia nchi nzima.

Dkt. Mwasaga amesema hiyo ni kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na Taasisi ya Umoja wa Mataifa (ITU).

Dokta Mwasaga ametaja mikakati ya kukuza uchumi wa kidigitali ikiwamo  kuhakikisha vifaa vya Tehama vinatengenezwa na kuundwa nchini kwa kuanzisha vituo vya ubunifu kwenye mikoa nane ya Arusha, Dodoma, Mwanza, Tanga, Lindi, Mbeya na Zanzibar.

"tunaendelea na ukamilishwaji wa vituo vya ubunifu TEHAMA (Soft centers) katika Kanda 5 pamoja na kuanzisha kituo kimoja Zanzibar". amesema 

Akizungumzia kuhusu teknolojia ya akili bandia, Mkurugenzi huyo amesema Tume kwa kushirikiana na baadhi ya vyuo vikuu nchini wameleta  kituo cha kuchakata taarifa zinazohusiana na masuala ya kijiografia ambacho awali kilikuwa Finland ili kukuza uchumi wa data.

"tunashirikiana na washirika wa maendeleo na kampuni za kimataifa katika kuendeleza bunifu za TEHAMA ikiwemo kuwezesha utengenezaji wa bidhaa za TEHAMA hapa nchini". amesema Dkt. Mwasaga

Msemaji Mkuu wa Serikali Gerson Msigwa ametoa wito kwa vijana kutumia fursa ya kuwekeza kwenye shughuli za  kidigitali.

"hiili ni jambo kubwa kwani fedha nyingi imewekezwa kwa ajili ya kuboresha TEHAMA nchini kwani shughuli mbalimbali kwa sasa duniani zinafanyika kwa njia ya kidijitali ikiwemo huduma za malipo mabalimbali, huduma za afya za matibabu, uzalishaji, kilimo, uchimbaji wa madini". amesema Msigwa

Tume ya TEHAMA katika mwaka wa fedha wa 2023/2024 imepanga kutekeleza mambo mbalimbali ikiwemo kuendelea na ukamilishwaji wa vituo vya ubunifu na kuanzisha kituo cha kutengeneza na kuboresha vifaa vya TEHAMA katika wilaya 10.

Post a Comment

Previous Post Next Post