TRILLIONI 1.7 KUTEKELEZA MIRADI MBALIMBALI YA NISHATI NCHINI-MHANDISI SAID
Na,Saleh Lujuo-Dodoma
Serikali imetoa jumla ya shilingi trillioni 1.7 kwa Wakala wa Nishati Vijiini (REA)kwaajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya nishati nchini.
Billion 12 zimetolewa pia kwa ajili ya mradi wa kuwezesha ujenzi wa vituo Vidogo vya kusambaza bidhaa za Petroli na Diseli vijijini Tanzania bara kwa lengo la Kulinda Mazingira na Afya ya Watumiaji pamoja na Kuboresha upatikanaji na Usambazaji wa Mafuta vijijini.
Mkurugenzi Mkuu Wa Wakala wa Nishati Vijiini REA Mhandisi Hassan Said amesema hayo leo Jijini Dodoma katika Mkutano na waandishi wa Habari ambapo amesema usambazaji wa mradi huo unahusu kuwekeza ujenzi wa vituo Vidogo vya mafuta Katika maeneo mbalimbali Vijiini.
"Tumeandaa programu maalumu ya kuhamasisha matumizi bora ya nishati na hii ni kuwaelimisha kina mama kwamba unaweza kitumia umeme kuzalisha mali ambapo upatikanaji wa umeme maeneo ya vijijini asilimia 69.6% vijiji 10600 vimefanikiwa kufikiwa tunamaliza kupeleka umeme kwenye vijiji sasa tunaanza kwenye vitongoji"Amesema Mhandisi Saidi.
Moja ya changamoto inayosababisha wananchi wasitumie nishati safi na kuendelea kutumia nishati ya asili yaani Mkaa na Kuni ni Pamoja na upatikanaji wake kwani nishati asilia zimekua zikipatikana kwa urahisi.
Mhandisi huyo amesema Wakala umeanza kutekeleza Mradi wa kusambaza mitungi ya gesi ya kupikia kwa utaratibu wa utoaji ruzuku kuwezesha usambazaji wa mitungi ya gesi ya kupikia (LPG) 71,000 yenye thamani ya shilingi bilioni 3 pamoja na majiko banifu 200,000 (laki mbili) katika maeneo ya vijijini huku Kwa Mwaka wa Fedha 2023/24 Jumla ya fedha takribani bilioni 10 zimetengwa kwaajili ya kufanikisha mradi huo.
"Tumefanikiwa kuja na programu ya kuwezesha majiko banifu na serikali imepata udhamini kutoka benki ya dunia kwa shilingi bilioni 14 pamoja na programu ya kuwezesha uzalishaji mkaa mbadala ili utumike badala ya kuni na mkaa"
Sambamba na hayo ametoa Rai kwa Watanzania kutumia mafundi wanaotambulika na Shirika la Umeme Tanzania ( TANESCO) na siyo kuwatumia mafundi vishoka wanaotumia njia za magendo kufanya shughuli hizo za uunganishaji wa Umeme.
"Tumedhamiria kuanzisha usambazaji wa mitungi ya gesi kila mkoa 2,700 na hii mitungi mtu anaweza kuiona ni midogo lakini tumekusudia kuhamasisha wananchi kutumia gesi na kuhamasisha wananchi kutoka kutumia mkaa na kuni ikiwa ni ajenda ya kutunza mazingira na kutoka kwenye nishati chafu hadi nishati safi" Amesisitiza Mhandisi Saidi
Kadhalika Serikali kupitia REA kwa kushirikiana na Benki ya Dunia (WB) imetenga Dola za Kimarekani (USD Milioni 6) kwa ajili ya mradi wa usambazaji wa majiko banifu ya kupikia.
Kabla ya Wakala wa Nishati Vijiini kuanzishwa nchini upatikanaji wa Umeme Vijiini uliku chini ya asilimia 5% na kufikia asilimia 69.6 za sasa.
Wakala wa Nishati Vijijini(REA)imedhamiria kuboresha maisha ya wananchi waishio vijijini kupitia upatikaji wa Nishati.