SERIKALI IMESHAANZA KUTEKELEZA AFUA YA MALEZI NA MAKUZI YA AWALI KATIKA VITUO MBALIMBALI NCHINI-DKT. GWAJIMA

SERIKALI IMESHAANZA KUTEKELEZA AFUA YA MALEZI NA MAKUZI YA AWALI KATIKA VITUO MBALIMBALI NCHINI-DKT. GWAJIMA

Na,Mwandishi wetu-Dodoma

Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt. Dorothy Gwajima amesema Malezi, Makuzi na Maendeleo ya  awali ya mtoto, Ajenda ya Taifa ya kuwekeza kwa vijana balehe na utekelezaji wa ahadi za nchi kwenye Jukwaa la usawa wa kijinsia ni baadhi ya maeneo yanayopewa kipaumbele katika utekelezaji wa afua mbalimbali kimkakati kutokana na umuhimu wake kwa jamii.

Waziri Gwajima ameyasema hayo jijini Dodoma Agosti 17, 2023 alipokutana kwa mazungumzo na   Mwakilishi mkazi wa Unicef nchini, Elke Wisch.

“Serikali  imekua mstari wa mbele katika kuboresha hali ya maisha kwa wananchi wake kwa kuja na    afua mbalimbali za Kimaendeleo zinazogusa makundi yote katika Jamii kupitia Maafisa Maendeleo na Ustawi wa Jamii japokuwa  changamoto ya  upungufu wa maafisa  bado ipo .

Amesema ili kuhakikisha tunakuwa  na Taifa lililo bora ni lazima kuanza kuwekeza kwa watoto na kwamba Serikali imeshaanza kutekeleza afua ya malezi na Makuzi ya awali katika  vituo kadhaa hivyo jitihada za kuongeza zinafanyika.

Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa Maendeleo ya Jamii,Jinsia ,Wanawake na Makundi Maalum Dkt. John Jingu amesema Serikali  imeendelea kutengeneza mazingira salama kwa watoto katika kuwainua wanawake.

“Kuimarisha hali ya uchumi kwa  wanawake ambao ni moja ya njia za kutengeneza mazingira bora  na salama kabisa kwa ajili ya Watoto nchini kwani wao ndiyo washiriki wakubwa wa malezi katika Jamii”. Amesema Dkt Jingu.

Naye, Elke Wisch ameahidi  Shirika hilo litaendelea kufanya kazi kwa ukaribu na Serikali ili kuhakikisha Taifa linafikia malengo yake katika kuboresha maisha ya Wananchi wake .

Post a Comment

Previous Post Next Post