KAMPENI YA SHAWISHIKA KUONGOZA KUPUNGUZA VITENDO VYA UKATILI NCHINI-DKT.DOROTHY GWAJIMA
ili kuongeza idadi ya Wasichana na Wanawake kwenye nafasi mbalimbali za Uongozi hapa nchini,Serikali imesema ipo haja ya kubadili fikra na mtazamo wa jamii kuhusiana na usawa wa kijinsia na uwezeshaji wanawake pamoja na kuongeza hali ya kujiamini kwa wanawake katika kushiriki katika nafasi za uongozi.
Serikali ya Tanzania pamoja Jumuiya ya Umoja wa Ulaya imesema kupitia Mpango wa mageuzi ya kijinsia,Vunja dari la kioo inatajwa Kutokomeza Ukatili wa Kijinsia,Kuwezesha Wanawake Kiuchumi na Kuelimisha Jamii kuhusiana na usawa wa kijinsia na umuhimu wa ushiriki wa wanawake na wasichana katika nyanja za kiuchumi, kisiasa na kijamii.
Akizindua kampeni ya Shawishika kuongoza leo juni 25,2025 jijini Dodoma,Waziri wa Maendeleo ya Jamii,Jinsia,wanawake na Makundi Maalum Dkt Doroth Gwajima amebainisha Lengo la Kampeni hiyo katika kuongeza idadi ya Wanawake na Wasichana katika Uongozi hapa nchini.
"Serikali kwa kushirikiana na Jumuiya ya Umoja wa Ulaya imeandaa kampeni ya inatekeleza Programu iitwayo Gender Transformative Action, Breaking the Glass Ceiling yenye malengo makuu matatu ambayo ni,Kutokomeza Ukatili wa Kijinsia,Kuwezesha Wanawake Kiuchumi,na Kuelimisha Jamii kuhusiana na usawa wa kijinsia na umuhimu wa ushiriki wa wanawake na wasichana katika nyanja za kiuchumi, kisiasa na kijamii". Amesema
Naibu katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii,Jinsia,wanawake na Makundi Maalum Wakili Amon Mpanju amesema kampeni hiyo itasaidia kuweka mizani sawa ya Wanawake na wanaume katika nguvu kazi na kusaidia kuleta Maendeleo ya Pamoja.
"Madhumuni yetu ni tuwe na jamii yenye uelewa, tuwe na wanawake wenye uthubutu na wenye kujiamini na tuongeze uwezo wa kujiamini kwa wasichana kuchukua masomo ya mchepuo wa sayansi, teknolojia, uhandisi na hisabati". Amesema Mpanju
ushirikiano kati ya serikali na Umoja wa Ulaya umekuwa na mchango mkubwa kupitia Mpango wa huu ,kama ambavyo Kaimu Balozi wa Umoja wa Ulaya Isabelle Mignucci amesema kampeni itahusisha sanaa za maagizo,Nyimbo,Video kuonesha umuhimu wa Mabadiliko.
"katika kutekeleza kampeni hii, moja kati ya mambo yatakayokuwa yanafanyika ni kufanya mahojiano na viongozi wanawake katika nyanja mbalimbali na kurekodi video fupi ambazo, zitakuwa zinarushwa kwenye vyombo vya habari". Amesema Issabele
Kampeni hiyo ni sehemu ya mpango wa Mageuzi ya kijinsia ,Vunja Dari la kioo 2021-2027 ambapo matarajio ni kuongeza Idadi ya wanawake katika uongozi kwenye sekta ambazo zinaonekana ni za wanaume peke yao,Kuongeza uelewa wa jamii kuhusiana na usawa wa kijinsia ,kupunguza vitendo vya ukatili na kuongeza idadi ya ushiriki wa wasichana na wanawake kwenye Masomo ya Sayansi nchini.


