HALMASHAURI KUU YA CCM TAIFA IMEPOKEA NA KUJADILI MAKUBALIANO YA UWEKEZAJI NA UENDESHAJI WA BANDARI.

HALMASHAURI KUU YA CCM TAIFA IMEPOKEA NA KUJADILI MAKUBALIANO YA UWEKEZAJI NA UENDESHAJI WA BANDARI.

Na,Saleh Lujuo-Dodoma.

Halmashauri kuu ya CCM Taifa ( NEC) imepokea na kujadili kwa kina taarifa ya makubaliano ya uwekezaji na uendeshaji wa bandari na kuazimia kwamba Uwekezaji na uendeshaji wa bandari hiyo ni kwa manufaa ya uchumi wa Nchi pamoja na utekelezaji wa vitendo vya ilani ya CCM ya Mwaka 2020 - 2025 ibara ya 59 ukurasa wa 92.

Akizungumza na waandishi wa habari Leo Julai 9,2023 jijini Dodoma Mara baada ya kumalizika Kwa kikao hicho, Katibu wa Halmashauri kuu ya CCM itikadi na Uenezi Sophia Mjema amesema halmashauri kuu ya Ccm imekutana Katika kikao Chake Cha kawaida chini ya mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.

"kikao hicho kimeazimia kwamba serikali iongeze kasi ya kutoa Elimu kwa wananchi juu ya uhalisia uliomo Katika makubaliano ya Uwekezaji na uendeshaji wa bandari". Amesema Mjema.

Halmashauri kuu ya CCM Taifa Kwa kauli Moja inazipongeza serikali zote mbili za chama cha mapinduzi, serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar chini ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi Kwa kuendelea kutafsiri Kwa vitendo ilani ya CCM ya mwaka 2020-2025 Kwa maslahi na ustawi wa watanzania wote.

Post a Comment

Previous Post Next Post