DKT.SAMIA SULUHU HASSAN MGENI RASMI KILELE CHA MADHIMISHO YA MIAKA 60 JKT.
Na,Saleh Lujuo-Dodoma
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh.Dkt.Samia Suluh Hassan anatarajiwa kuwa mgeni Rasmi katika Kilele cha Maandhimisho ya Miaka 60 ya JKT ambayo yatafanyika tarehe 10 Julai 2023 Jijini Dodoma.
Akizungumza na waandishi wa Habari Leo Jul 8.2022 jijini Dodoma Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Mhe. Innocent Bashungwa anawaalika viongozi wote wa Serikali, Taasisi mbalimbali za umma na binafsi, watumishi, wananchi wa Mkoa wa Dodoma na Watanzania kwa ujumla kujitokeza kwa wingi kuhudhuria siku ya kilele cha Maadhimisho haya.
"Katika maadhimisho hayo, kutakuwa na gwaride la vijana wa JKT, maonesho ya vifaa mbalimbali vya SUMAJKT na burudani za NGOMA kutoka vikundi vya JKT na Wasanii mbalimbali". Amesema Bashungwa.
Aidha Mhe.Bashungwa amesema katika kilele cha Maadhimisho ya Miaka 60 ya JKT kulifanyika Shughuli mbalimbali ikiwemo JKT Marathon 2023 yaliyofanyia June 25 pamoja na uzinduzi wa Mnara wa kumbukumbu uliopo makao makuu ya JKT Dodoma Chamwino.
"Kilele cha Maadhimisho ya Miaka 60 ya JKT, kimetanguliwa na shughuli mbalimbali ikiwa ni pamoja na JKT Marathon 2023 iliyofanyika Juni 25 hapa Dodoma, kuzinduliwa kwa Mnara wa kumbukumbu katika Makao Makuu ya JKT (Chamwino Dodoma), kufunguliwa kwa maonesho ya bidhaa ambayo yanaendelea hadi sasa katika viwanja vya Medeli East mkabala na SUMAJKT House na kushiriki katika huduma za kijamii kama kutembelea hospitali ya Uhuru iliyopo wilayani Chamwino pamoja na vituo vya kulelea watoto wenye uhitaji". Amesema Bashungwa.
Kilele cha Maadhimisho ya Miaka 60 ya JKT kinatarajiwa kuadhimishwa rasmi ifikapo tarehe 10 Julai, 2023 ambapo Mgeni Rasmi atakuwa ni Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu.