ZAIDI YA WATU MILLION 2.9 HUPOTEZA MAISHA DUNIANI KOTE KUTOKANA NA AJALI NA MAGONJWA YATOKANAYO NA KAZI


Takwimu zinaonesha nchi Tanzania jumla ya ajali na magonjwa yaliyoripotiwa katika Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi kuanzia Julai 2019 hadi Juni 2021 ni ajali 4,993 na magonjwa 249 Katika ajali hizo vifo vilikuwa 217.

Takwimu hizo amezitoa waziri Wa Nchi ofisi ya waziri Mkuu kazi,vijana,ajira na wenye ulemavu Mh Prof Joyce ndalichako Leo  April 26.2023 jijini Dodoma wakati akizungumza na waandishi Wa Habari kuhusu Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Usalama na Afya Mahali pa kazi ambayo huadhimishwa Tarehe 28 Aprili kila mwaka ambapo amesema Takwimu za kidunia zilizotolewa na Shirika la Kazi Duniani mwaka 2022 zinaonesha kwamba zaidi ya watu milioni mbili na laki tisa(2.9) hupoteza maisha kutokana na ajali na magonjwa yatokanayo na kazi.

"Takwimu hizo ni kubwa sana zinaathiri utendaji kwa kuwa zinasababisha upotevu wa maisha ya Wafanyakazi na pia kuathiri shughuli wakati wafanyakazi walioumia wakiendelea kupata matibabu.Kwa mantiki hiyo, ni dhahiri kwamba suala la ajali na magonjwa yatokanayo na kazi linahitaji jitihada za makusudi katika kukabiliana nalo. Serikali ya JMT inatambua umuhimu wa kulinda NguvuKazi ya Taifa na Kupitia Taasisi yake ya OSHA 
Serikali inaendelea kusimamia kwa karibu utekelezaji wa Sheria Na. 5 ya Afya na Usalama Mahali pa Kazi ya mwaka 2003 miongoni mwa wadau na Watanzania wote kwa ujumla ambapo Lengo ni kuhakikisha kwamba maeneo yote ya kazi Nchini yanakuwa na mifumo madhubuti ya kuwakinga wafanyakazi dhidi ya ajali na 
magonjwa yatokanayo na kazi" Amesema Prof Ndalichako.

Kwa  upande wake Mtendaji Mkuu wa Wakala wa usalama na afya mahala pa kazi,Hadija Mwenda amesema kuwa kutokana na utafiti mdogo walioufanya wamebaini ajali nyingi kazini zimekuwa zikitokea katika Sekta ya uzalishaji kwa maana ya Viwanda.

Naye Rais wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi  Tanzania(TUCTA)Tumaini Nyamhokya ameiomba Serikali  kuweka Sheria kali ambazo zitawabana Waajiri kuzingatia  masuala ya usalama mahala pa kazi.

Mwakilishi wa Shirika la kazi Duniani( ILO) Getrude  Sima amesema wataendelea kushirkiana na serikali ya Tanzaniana kuitaka kuendelea kutumia sheria namba tano ya usalama mahala pa kazi.

Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Usalama na Afya Mahali pa kazi ambayo huadhimishwa Tarehe 28 Aprili kila mwaka Kwa Mwaka 2023 yataadhimishwa Mkoani Morogoro yakiambatana na kauli mbiu isemayo Mazingira Salama na Afya kazini ni Kanuni na Haki ya 
Msingi Mahali pa Kazi” (A Safe and Health Working 
Environment is a Fundamental Principle and Right at Work) ambapo  Tanzania ilianza kuazimisha  kwa mara ya kwanza mwaka 2004.


Post a Comment

Previous Post Next Post