Na,Mwandishi wetu Dodoma.
Tume ya nguvu za Atomiki nchini,imetakiwa kuwekeza zaidi katika utafiti ili kupata bunifu nyingi hasa kwenye eneo la Sayansi ya Nyuklia kwani ni muhimu sana katika ulimwengu wa sasa wa teknolojia kwa lengo la kukuza uchumi wa nchi.
Mkurugenzi wa idara ya sayansi na teknolojia wa Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia Prof Maulilio Kipanyula ametoa wito huo leo April 27.2023 Jijini Dodoma kwaniaba ya Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya elimu wakati wa siku ya atomiki kwenye maonyesho ya wiki ya ubunifu iliyoambatana na maandamano yaliyofanyika viwanja vya Jamhuri Jijini Dodoma ambapo Amesema Sayansi ya nyuklia ni eneo muhimu sana katika kukuza uchumi na Taifa Kwa ujumla.
"hili eneo ni muhimu sana katika ulimwengu Wa Sasa Wa Teknolojia Kwa lengo la kukuza uchumi Wa nchi lakini pia kupata wabunigu hodari katika eneo hili ili Taifa liwe na wataalamu wenye uwezo mkubwa katika masuala ya nyuklia" Amesema Prof Maulilio.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi wa Tume hiyo,Prof Joseph Msambichaka ameitaka tume ya Atomiki kufanya bunifu nyingi zinazotokana na nyuklia kwani Tume hiyo ina uhitaji wa vifaa vingi vyakutosha.
Naye Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Atomiki Prof Lazaro Busagala amesema kuwa hapo baadae wanatarajia kuwa na uwakilishi mkubwa wa wanawake katika sayansi na teknolojia hasa ya nyuklia ambapo hivi sasa wametenga jumla ya Shilingi bilioni 2.6 kwaajili ya kuwasomesha wanafunzi ambao wamefanya vizuri katika shahada zao kupitia mpango mkakati wa dokta Samia scholarship ili kupata wabunifu zaidi.
"Kwa sasa kwenye suala Zima la wanawake katika Sayansi na Teknolojia ni wachache sana hivyo tunatarajia kwenye eneo hili la nyuklia kuongeza idadi kubwa ya wanawake ambapo tumetenga jumla ya shillingi Billion 2.6 kwaajili ya kuwasomesha wanafunzi ambapo wamefanya vizuri katika shahada zao kupitia Mpango Mkakati Wa Dokta Samia scholarship ili kupata wabunifu zaid" Amesema Prof Lazaro.
ikumbukwe kuwa Mionzi inafaidi nyingi Kwa Maendeleo na ustawi katika jamii,inatumika kwenye sekta mbalimbali ikiwemo Afya,kilimo,Mifugo na viwanda lakini pamoja na kuwa na faida nyingi isipotumika inavyotakiwa inaweza kuingia katika Mnyororo Wa chakula ambapo ni hatari Kwa Afya ya Binadamu na wanyama.


