Na,Saleh lujuo Dodoma.Jamii imeshauriwa kutumia Mifumo ya ndani ya nchi yakimawasiliano ili kurahisisha kutoa huduma Kwa haraka na kuratibu shughuli za kimawasiliano Kwa kupiga simu Kwa Taasisi mbalimbali za umma ikiwemo Mfumo Wa mawasiliano intergrated call center na CRM.
Akizungumza na waandishi Wa Habari katika kilele Cha Maadhimisho ya wiki ya Ubunifu kitaifa Leo April 28.2023 Jijini Dodoma Afisa TEHAMA Wa Mamlaka ya serikali Mtandao Tumaini Masinsi Amesema Mfumo huo ni mahususi kwa ajili kuongeza ufanisi wakuhudumia wananchi wenye malalamiko, maulizo mapendekezo, na pongezi
"Intergrated CallCenter System & CRM
Ni mfumo wa kuratibu shughuli za kimawasiliano kwa kupiga simu kwa Taasisi mbalimbali za Umma,Mfumo huu ni mahususi kwa ajili kuongeza ufanisi wakuhudumia wananchi wenye malalamiko, maulizo mapendekezo, na pongezi" Amesema Masinsi.
Aidha,Amesema Mfumo Wa ChatAI nao
Ni ubunifu unaotumia teknolojia ya akili bandia kusaidia Mamlaka ya Serikali Mtandao kujibu maswali ya mara kwa mara kuhusiana na utendaji kazi wa Mamlaka.
"Mfumo huu unapatikana kupitia ega.bot.all.co.tz na Mfumo mwingine Wa Sec doc Ni ubunifu wa mtandao unaotokana na teknolojia ya blockchain yenye malengo ya kuongeza ulinzi kwenye matumizi na utumaji wa nyaraka mbalimbali" Amesema Masinsi.
Sambamba na Hayo amewataka Watanzania kutumia Mfumo Wa eMrejesho ambapo Ni mfumo wa kutuma, kupokea na kufuatilia malalamiko, mapendekezo, maulizo na pongezi kwenda kwa taasisi mbalimbali za umma.
"Mfumo huu unapatika kwa njia ya web “eMrejesho.gov.go.tz” njia ya mobile application kwa Playstore na Applestore kwa jina la mrejesho pia kwa njia ya msimbo *152*00# kisha namba 9, kisha namba 2" Amesema Masinsi.
Kwa upande wake Afisa TEHAMA Wa Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi Wa umma na utawala Bora Osea laizer Amesema bunifu hizo zimelenga kusaidia makundi mbalimbali wakiwemo watumishi Wa umma.