Waziri wa Mifugo na Uvuvi,Mhe.Abdallah Ulega amezindua matreka mapya matano (5) na kupokea ngo'mbe elfu moja (1000) kwa ajili ya kuboresha uzalishaji wa kampuni ya NARCO katika katika Ranchi ya Kongwa
Akizungumza wakati wa ziara yake,Leo Aprili 27,2023 jijini Dodoma,aliyoifanya katika Ranchi ya Kongwa iliyopo Wilayani Kongwa amesema Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan imeiwezesha Kampuni ya Ranchi za Taifa (NARCO) kiasi cha Shilingi bilioni 4.65 kwa ajili ya kununua vitendea kazi na ng'ombe wazazi ili kuboresha na kuongeza uzalishaji wa kampuni hiyo.
Aidha amesema lengo la Serikali ya awamu ya sita ni kuiimarisha NARCO kwa kuboresha miundombinu na vitendea kazi ili waweze kunenepesha ng'ombe, kuimarisha biashara ya nyama bora ya Kongwa Beef na kuzalisha malisho ya mifugo kwa wingi na kuyauza ndani na nje ya nchi.
"lengo la Serikali ya awamu ya sita ni kuiimarisha NARCO kwa kuboresha miundombinu na vitendea kazi ili waweze kunenepesha ng'ombe, kuimarisha biashara ya nyama bora ya Kongwa Beef na kuzalisha malisho ya mifugo kwa wingi na kuyauza ndani na nje ya nchi",amesema.
Kwa upande wake,Mtendaji Mkuu wa Narco,Profesa Msofe amesema malengo ya Narco ni kuendeleza Narco,kuzalisha mifugo bora,kuzalisha malisho,kununua mifugo kutoka kwa wananchi na kisha kuinenepesha,kuhifadhi mazingira na Kongwa kuwa ranchi ya mfano.
Prof Msofe amesema katika mwaka wa fedha,2022-2023,Serikali ilitenga Sh 4.65 bilioni kwa ajili ya kuboresha na kuongeza uzalishaji katika ranchi za Kongwa na Mzeri.
Amesema fedha hizo zilitengwa kwa ajili ya kununulia ng'ombe wazazi,vifaa vya shamba na uchimbaji wa visima virefu.
Katika ziara hiyo,Waziri Ulega alikagua matrekta,vifaa vitakavyotumika kuvunia malisho ya mifugo ambayo vimetolewa na Serikali na kisha alizungumza na wananchi wanaoishi jirani na ranchi hiyo.