MAPATO YA UTALII YAONGEZEKA KUTOKA TRILIONI 3.01 MWAKA 2021 HADI TRILLIONI 5.82.


Na saleh lujuo Dodoma.

Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii,Dkt.Hassan Abbasi amesema mapato ya utalii yaongezeka maradufu kutokana na watalii kuongezeka nchini ikiwa ni matunda ya Royal Tour, ambapo mapato ya jumla ya sekta ya utalii yameongezeka kutoka Trilioni 3.01 mwaka 2021 hadi Trilioni 5.82 na kuifanyaTANAPA na NCAA kuvunja rekodi ya mapato.

Dkt Abbasi ametoa Takwimu hizo leo Aprili 28,2023 jijini Dodoma wakati akielezea mafanikio ya  mwaka mmoja tangu Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, alipozindua jijini Arusha na hatimaye watanzania wengi kuiona kwa mara ya kwanza filamu ya “TANZANIA; THE ROYAL TOUR.”

Aidha ameeleza jinsi ROYAL TOUR ilivyojenga hamasa kwa watalii na wawekezaji, sasa hamasahiyo pia imekuwa na manufaa kwa sekta ya usafiri wa Anga kama takwimu za Manufaa kwa Uwanja wa Kimataifa wa Kilimanjaro pekee kama sampuli ya ndege za Kimataifa Zaongeza Ruti Tanzania Miruko ya jumla ya ndege za kimataifa KIA iliongezeka kwa asilimia 28 kutoka miruko 6,115 April 2021 hadi 7,850 April, 2023.

"kutokana na watalii kuongezeka nchini ikiwa ni matunda ya Royal Tour, mapato ya jumla ya sekta hii yameongezeka kutoka Dola za Marekani 1.310.34 (Sawa na TZS Trilioni 3.01) mwaka 2021 hadi Dola za Marekani,527.77 (sawa la TZS Trilioni 5.82) imefanya Tanapa na NCAA wamevunja rekodi ya mapato"Amesema Dkt Abbasi.

Ushiriki wa Mhe. Rais Dkt Samia suluhu hasan katika filamu ya Royal Tour umeleta mafanikio ambapo Novemba mwaka jana huko Dallas, Texas, USA, Taasisi ya Tuzo za Afrimma ilimtangaza Rais Samia  Suluhu Hassan kuwa Rais Mwanamke wa kwanza Afrika Kushinda Tuzo ya Mageuzi Katika Uongozi wakitamka bayana kuwa mojawapo ya vigezo na mafanikio ni ushiriki wake katika Royal Tour.

Dkt Abbasi Amesema Royal Tour sio mwisho ni mwanzo wa kuitangaza nchi kimataifa zaidi hivyo Kamati ya mwaka mmoja sasa, imepokea na inaendelea kuchambua “Royal Tours” nyingine zijazo na Maombi Kujitangaza Ligi Kubwa za Ulaya na Marekani  Kutokana na hamasa ya Royal Tour klabu mbalimbali za Ligi Kubwa Duniani hasa Uingereza, Hispania na Marekani wapo katika mazungumzo nazo na wameshapokea ofa zao.

Ushiriki wa Mhe. Rais Dkt Samia suluhu hasani katika filamu ya Royal Tour umeleta mafanikio ambapo Novemba mwaka jana huko Dallas,Texas, USA, Taasisi ya Tuzo za Afrimma ilimtangaza Rais Samia  Suluhu Hassan kuwa Rais Mwanamke wa kwanza Afrika Kushinda Tuzo ya Mageuzi Katika Uongozi wakitamka bayana kuwa mojawapo ya vigezo na mafanikio ni ushiriki wake katika Royal Tour",amesema Abbasi.


Post a Comment

Previous Post Next Post