DODOMA
💧SERIKALI Awamu ya Sita chini ya Uongozi wa Rais Dk. Samia Suluhu Hassan kupitia Mamlaka ya Rufani ya Zabuni za Umma (PPAA) imeokoa Shilingi bilioni 586.5 baada ya kuzuia utoaji wa tuzo za Zabuni 43 zilizokuwa zimetolewa kwa wazabuni waliokosa uwezo wa kifedha na sifa za kitaalamu za kutekeleza miradi husika.
hatua hii ni utekelezaji usioridhisha wa miradi ambao ungesababisha upotevu wa fedha za umma na kuchelewesha maendeleo endelevu na stahiki kwa wananchi.
Hayo yamebainishwa Jijini Dodoma leo Februari 25,2026 na Katibu Mtendaji wa PPAA, James Sando, wakati wa mkutano wake na waandishi wa Habari Kuhusu siku.100 za Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Amesema kupitia kitengo cha rufaa, Mamlaka imesajili mashauri 196 yaliyotokana na michakato mbalimbali ya ununuzi wa umma ambapo Kati ya mashauri hayo, zabuni 43 zenye thamani ya Shilingi bilioni 586.5 zimezuiwa kutolewa kutokana na wazabuni husika kutokidhi vigezo vya kifedha na kitaalamu.
"Usuluhishi wa migogoro hauwezi kufanikishwa katika mazingira ya ubaguzi wala pale ambapo fursa na haki za kiuchumi na kiraia hazitolewi kwa usawa". Amesema
"hivyo, hatua ya Mamlaka ya Rufani kuzuia utoaji wa tuzo kwa wazabuji 43 waliokosa sifa za kutekeleza zabuni, inaimarisha mchakato wa usuluhishi wa migogoro na ni moja ya falsafa nne za Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan". Ameongeza
Kadhalika,Katibu Mtendaji huyo amesema katika kuimarisha uwazi, uwajibikaji na ufanisi katika sekta ya ununuzi wa umma, Mamlaka hiyo imekamilisha moduli ya kupokea na kushughulikia malalamiko na rufaa kwa njia ya kielektroniki kupitia Mfumo wa Ununuzi wa Umma kwa Njia ya Kielektroniki (NeST).
"Moduli hiyo imerahisisha usajili na ushughulikiaji wa malalamiko na rufaa, na kuongeza uwazi katika mchakato wa ununuzi wa umma". Amesema
“Tangu kuanza kutumika kwake, jumla ya malalamiko 549 yamewasilishwa na kushughulikiwa na taasisi nunuzi, huku rufaa 26 zikiwasilishwa na kuamuliwa na Mamlaka ya Rufani kupitia mfumo huo". Ameongeza
Mamlaka ya Rufani inasimamia Utawala Bora kupitia utatuzi wa migogoro inayowasilishwa mbele yake Kwa kuhakikisha kuwa zabuni zinazotolewa Kwa wazabuni wenye sifa na uwezo stahiki katika kufanya utekelezaji au kazi husika ilu kuiwezesha serikali kupata thamani halisi ya Fedha katika ununuzi wa umma na kuharakisha upatikanaji wa huduma mbalimbali Kwa wananchi.

