TUSHIRIKI UCHAGUZI KWA AMANI - DKT SAADA MKUYA


TUSHIRIKI UCHAGUZI KWA AMANI - DKT SAADA MKUYA

Na Mwandishi wetu 

Waziri wa nchi ofisi ya Rais Fedha na Mipango Zanzibar ataka amani na utulivu uchaguzi  Oktoba 29

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - Fedha na Mipango Zanzibar Dkt  Saada Mkuya Salum amesema uchaguzi bila vurugu Inawezekana hivyo amewataka waTanzania wote kushiriki zoezi Hilo bila kuvunja Sheria kwani wakipata madhara bima haziwezi kuwasaidia.

Hata hivyo mhe Saada Mkuya Salum amewaagiza wadau wa Bima kushirikiana kwa karibu na serikali kupitia mamlaka ya usimamizi wa bima TIRA,wizara ya afya na taasisi nyingine husika ili  kuhakikisha utekelezaji wa sheria ya Bima ya afya kwa wote inakwenda kwa kasi na ufanisi.

Kadhalika amewataka TIRA Kuendelea kuelimisha umma kuhusu umuhimu wa Bima ya afya hasa katika maeneo ya vijijini.

Aidha ameitaka Mamlaka ya usimamizi wa Bima kuhakikisha inaongeza ubunifu zaidi katika kusimamia sekta ya Bima hususani eneo la ushughulikiaji wa madai.

Ameongeza kuwa pamoja na kazi zingine mamlaka ya usimamizi wa Bima imeweza kutoa miongozo ya ukusanyaji na utozaji wa ada za Bima.

Post a Comment

Previous Post Next Post