SERIKALI IMEDHAMIRIA KUDHIBITI MAGONJWA YA MIFUGO ILI KUONGEZA UZALISHAJI-DKT. KIJAJI
Na,Saleh Lujuo-Dodoma
Waziri wa Mifugo na Uvuvi Dkt. Ashatu Kijaji amesema Serikali inatambua umuhimu wa kudhibiti magonjwa ya mifugo ili kuongeza uzalishaji wa mifugo na mazao yake na kuimarisha afya ya wanyama sambamba na kudhibiti magonjwa kwa kuwezesha upatikanaji na usambazaji wa chanjo mbalimbali nchini ikiwemo kusimamia na kutoa elimu kwa wadau.
Waziri Kijaji amesema hayo leo May 6,2025 jijini Dodoma wakati akitoa taarifa ya mafanikio na mwelekeo wa Wizara hiyo ndani ya kipindi cha miaka minne ya Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Waziri Dkt. Kijaji ameongeza kwamba katika kuendelea kuimarisha afya ya mifugo nchini Serikali inatarajia kuzindua kampeini ya Chanjo ya mifugo Kitaifa kati ya mwezi Mei hadi Juni 2025.
"zitatolewa dozi 17,224,200 za chanjo ya Sotoka ya Mbuzi na Kondoo kwa ajili yakuchanja zimenunuliwa na zinatarajia kuchanja jumla ya ng’ombe 19,099,100;naJumla ya
jumla ya dozi 19,099,100 za chanjo ya Homa ya Mapafu ya Ngombe (CBPP) na Uchanjaji huu, utaiwezesha Tanzania kukidhi masharti ya biashara ya mifugo na mazao yake kulingana na matakwa ya Shirika la Afya ya Wanyama Duniani". Amesema
Katika kipindi cha miaka minne(4) kuanzia mwaka 2021/22 hadi mwaka 2024/25,bajeti ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi imeendelea kuongezeka kutoka shilingi 169,194,996,999 mwaka 2021/22 hadi shilingi 460,333,602,000 mwaka 2024/25.



