WMA YAKATAA VIPIMO 5,607 VYENYE MAPUNGUFU YASIYO REKEBISHIKA.


WMA YAKATAA VIPIMO 5,607 VYENYE MAPUNGUFU YASIYO REKEBISHIKA.

Na,Deborah Lemmubi-Dodoma.

Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Vipimo (WMA) Bwana Alban Kihula amesema kuwa Wakala hiyo ilipanga kuhakiki Vipimo 3,923,652 vitumikavyo katika Sekta mbalimbali na imefanikiwa kuhakiki Vipimo 3,668,149 sawa na asilimia 94 ya lengo.

 Bwana  Kihula ameyasema hayo leo Machi 2025 wakati akizungumza na Waandishi wa Habari Jijini Dodoma akielezea Mafanikio na Mwelekeo wa Wakala wa Vipimo katika Maadhimisho ya miaka minne ya Serikali ya Awamu ya Sita.

 "Katika kipindi cha miaka minne ya Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan Wakala ilipanga kuhakiki vipimo 3,923,652 vitumikavyo katika Sekta mbalimbali nchini na imefanikiwa kuhakiki vipimo 3,668,149 sawa na asilimia 94 ya lengo".

"Kati ya vipimo hivyo vilivyohakikiwa, vipimo 102,969 vilikutwa na mapungufu ambayo yalirekebishwa na kuruhusiwa kuendelea kutumika na vipimo 5,607 vilikataliwa kutumika baada ya kuonekena na mapungufu ambayo hayarekebishiki ".

 Pamoja  na hilo Mtendaji Mkuu wa Wakala hiyo amesema kwenye  vifaa vya ujenzi pia,WMA wanaendelea kufanya kaguzi ili kuthibiti uchakachuaji wa vifaa hivyo.

“Kwenye vifaa vya ujenzi tumeendelea kufanya kaguzi kali sana changamoto ambayo tunayo hatuwezi tukawa tunatangaza kila kaguzi unaweza kukuta ni kiwanda kikubwa lakini kuna mfanyakazi mmoja tu anataka kuharibu taswira ya kiwanda.

 "Kwahiyo tunachukua hatua kwenye vifaa vya ujenzi tumekuwa wakali sana kuliko muda wowote kwenye nondo kwenye saruji ujazaji wa rangi na vifaa vingine vya ujenzi".

Post a Comment

Previous Post Next Post