TIB NA UNIDO ZAHAMASISHA MATUMIZI NISHATI SAFI NCHINI.

TIB NA UNIDO ZAHAMASISHA MATUMIZI NISHATI SAFI NCHINI.

Na Deborah Lemmubi-Dodoma.

Benki Ya Maendeleo TIB, Kwa Kushirikiana Na Shirika La Umoja Wa Mataifa La Maendeleo Ya Viwanda (Unido), Inatekeleza Mpango Wa Kuhamasisha Matumizi Ya Nishati Safi Ya Kupikia hapa Nchini.

Hayo yameelezwa Jijini Dodoma Na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Wa TIB,Bi. Lilian Mbassy, Wakati Akizungumza Na Waandishi Wa Habari Kuelezea mafanikio Ya Taasisi Hiyo katika kipindi cha Miaka Minne Ya Serikali Ya Awamu Ya Sita chini ya Mhe Dkt Samia. 

Amesema Rais Samia, Ni Kinara Wa Nishati Safi Ya Kupikia,Hivyo TIB Wameshirikiana Na Unido Katika Mradi Wa Kuhamasisha Matumizi Ya Nishati Inayotokana Na Mabaki Ya Miwa.

"Kupitia mradi wa 'Waste to energy' Benki itaendelea kushirikiana na Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo ya Viwanda UNIDO katika matumizi ua Nishati safi".

kaimu Mkurugenzi Mtendaji Huyo Ameongeza Kuwa Benki Hiyo Imefanya Uwekezaji Katika Mamlaka Za Maji Uliosaidia Kumtua Mama Ndoo Kichwani Kwa Kufikisha Huduma Ya Maji Safi Na Salama Karibu Na Makazi Ya Wananchi, Hasa Vijijini.

Akizungumzia Vipaumbele Vya Benki Hiyo Kwa Mwaka 2025 Amesema Vimejikita Katika Kuunga Mkono Juhudi Za Serikali Katika Kutekeleza Sera Na Mikakati Ya Kitaifa Ili Kuongeza Kasi Ya Mendeleo Pamoja Na Kutekeleza Vipaumbele Vya Serikali Ya Awamu ya Sita.

Post a Comment

Previous Post Next Post