PASS LEASING NI MFANO WA KUIGWA-RC SENYAMULE


PASS LEASING NI MFANO WA KUIGWA-RC SENYAMULE

Na,Saleh Lujuo-Dodoma

Kutokana na serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kuwatengenezea Mazingira wezeshi wakulima ili wazalishe kwa tija, wasambazaji wa matrekta ya new holland kwa kushirikiana na kampuni ya pass leasing wamegawa matrekta  kwa wakulima 12 kutoka sehemu  mbalimbali ikiwemo Mkoa wa Dodoma.

Lengo la Pass leasing ni kuwawezesha wakulima wote nchini ambapo Matrekta hayo yanaenda kufanya kazi nchi nzima na takribani wakulima 700 watanufaika na matrekta hayo.

Akizungumza Mara baada ya kukakabidhi matrekta hayo Mkuu wa mkoa wa Dodoma , Rosemary Senyamule katika viwanja vya maonesho 88 jijini Dodoma amesema dhamira ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ni kuwawezesha wakulima kupata vifaa vitakavyo wasaidia katika shughuli zao za kilimo.

"Makubwa yanayofanyika kwenye sekta ya kilimo ni makubwa na tayari vijana wameendelea kuwezesha katikati sekta ya kilimo ,hivyo niwapongeze kampuni ya  PASS leasing kwa kuweza kuwapatia wakulima vifaa vya kisasa na kuwatoa kwenye kilimo cha mkono ambacho kinatumia muda mwingi". Amesema

"Kampuni ya PASS leasing kwa kweli niwapongeze sana na kugawa matreka haya  12 kwa wakulima ni jambo la kipee sana ambapo matrekta haya yataenda kuleta matokeo chanya kwenye kilimo kwa kusaidia kuleta mapinduzi makubwa kwenye sekta ya kilimo". Ameongeza

Kadhalika, amesema maonesho haya ya 88 kwa kanda ya kati Dodoma yataendelea ili kuwapa fursa wananchi hususani wakulima kuja kuendelea kujifunza shughuli mbalimbali za kilimo.

Killo Lussewa, ni Mkurugenzi mtendaji wa PASS Leasing amesema dhamira ya kampuni hiyo ni moja ya majukumu yao ya kuwasaidia wakulima na tayari hadi sasa takriban wakulima 1200 wamefikiwa. 

"Kampuni ya PASS Leasing, leo imekabidhi vifaa vya kulimia, ambavyo ni trekta 9 aina ya New Holland TT75-4WD, machine ya kupura mahindi na gari 1 aina FAW zenye themani ya TZS 755.5 millioni kwa wakulima wa mkoa wa Dodoma na Singida;waliowezeshwa kupitia huduma za PASS Leasing"

"Uwezeshaji huu tunategemea utakwenda kuongeza uzalishaji kwa kulima mashamba zaidi ya ekari 4000 na ujenzi na usambazaji wa kiwanda cha viwatilifu; kutengeneza ajira za moja kwa moja zisizopungua 65 na kuwafikia wanufaika  takribani 700 kwa kipindi cha msimu mmoja"Amesema

"Aidha, katika kanda ya kati, mkoa wa Dodoma na Singida wamewawezesha zana zenye jumla ya thamani ya takribani ya bilioni 20 kwa wajasiliamali takribani  400 kati yao vijana ni 25%.

Boniface Mollel ambaye ni Afisa masoko wa Hughes Agriculture Limited  amesema waliokabidhiwa matreka hayo watapewa pia vifaa vingine kwa ajili matengenezo.

Minza mlela Mkulima kutoka chamwino ambaye amekabidhiwa trekta  amesema Matrekta hayo yatawasaidia kufanya kazi za kilimo kwa haraka na zitawaongezea kipato kwa kukodishia  wakulima wengine.



Ikumbukwe kuwa Dhamira kuu ya kampuni ya PASS Leasing ni Kuhakikisha wazalishaji wa kilimo wanafikia uwezo wao mkubwa kupitia ufadhili wa kukodisha/kukopeshwa vifaa kwa bei nafuu.

Post a Comment

Previous Post Next Post