MICHEZO HUSAIDIA VIJANA KUJIEPUSHA NA MATENDO MAOVU-PROF. MKENDA


MICHEZO HUSAIDIA VIJANA KUJIEPUSHA NA MATENDO MAOVU-PROF. MKENDA

Imeelezwa serikali  kuwa itahakikisha michezo inaendelezwa shuleni kwa sababu inasaidia vijana kujihepusha na matendo yasiyofaa.

Hayo yamesemwa hii Julai 20, 2024 na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda wakati wa ufunguzi wa mashindano ya mpira wa miguu ya Wazazi Dar es salaam Super Cup yaliyoanza kutimua vumbi rasmi katika viwanja vya Bandari Jijini Dar es salaam, 

Mkenda ameongeza kuwa hakuna namna ya kutenganisha Shughuli za Elimu na Jumuia ya Wazazi huku akiahidi kuwa ataendele kushirikiana na Jumuiya ya wazazi Taifa na Jumuiya ya wazazi Dar es salaam wakati wowote akihitajika.

Amepongeza Jumuiya wa Wazazi Dar es salaam kwa juhudi kubwa za kuanzisha na kuendeleza michuano.

Naye Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Mkoa wa Dar esw salaam Bi. Khadija Ally Said amesema  mashindano hayo yana  lengo la kukuza vipaji vya vijana pamoja na kuleta malezi chanya kwenye jamii.

Vile vile ameongeza kuwa mashindano hayo yanawaandaa vijan kuelekea kwenye Uchaguzi wa viongozi wa Serikali za mitaa pamoja na kujiandikisha kwenye daftari la kudumu la wapiga kura.

Bi. Khadija amesema kupitia michezo hiyo vijana wanapata ajira pamoja na kiwaunganisha na kupata fursa ya kubadilisha mawazo lakini pia  inawaunganisha wazazi.

Uzinduzi huu umeambatana na zoezi la kuchangia damu na jamii imepata nafasi ya kupima ugonjwa wa Seli Mundu.

Mshindi wa kwanza wa mashindano hayo atajinyakulia kitita cha shilingi milioni tano, mshindi wa pili milioni tatu na mshindi wa tatu milioni mbili.








Post a Comment

Previous Post Next Post