VIFAA TIBA NI MSINGI WA HUDUMA ZA UHAKIKA NA HUDUMA BORA-DKT.JINGU


VIFAA TIBA NI MSINGI WA HUDUMA ZA UHAKIKA NA HUDUMA BORA-DKT.JINGU

Na,Saleh Lujuo-Dodoma

Katibu Mkuu Wizara ya Afya,Dkt.John Jingu ameagiza kuimarishwa kwa idara ya uhandisi vifaa tiba ndani ya hospital kiuwezo na kitaaluma katika kuweza kutatua na kufanya matengenezo tiba na matengenezo Kinga ya vifaa tiba katika hospital  hapa nchini.

Kauli hiyo ameitoa Dkt.John Jingu leo Jijini Dodoma wakati akipokea vifaa vya hewa  tiba ya Oxygen  vilivyotolewa na Taasisi isiyo ya kiserikali ya CLINTON HEALTH ACCESS INITIATIVE (CHAI) ambapo amesema uwepo wa vifaa tiba ni msingi wa huduma za uhakika na huduma Bora.


Kwa upande wake Dkt. Esther Mtumbuka, Mkurugenzi Mkaazi Taasisi isiyo ya kiserikali ya CLINTON HEALTH ACCESS INITIATIVE (CHAI) amesema taasisi hiyo kwa kushirikiana na wizara ya Afya imewawezesha mainjinia na viongozi wa hospital kupata taarifa juu ya mwenendo wa  vifaa tiba vyote ambavyo vipo Kwenye hospital zao.


Maria Mtuya Mhandisi vifaa tiba hospital ya Rufaa Kanda ya Mbeya amesema taasisi ya CHAI ni taasisi ambayo imewajengea uwezo watalam wa Afya katika hospital Rufaa Kanda ya Mbeya hivyo kupitia ujuzi waliopata wapo tayari kwenda kutoa ujuzi huo katika hospital za wilaya ili zipate uelewa Juu ya kufanya matengenezo tiba na matengenezo Kinga ya vifaa tiba katika hospital  zao.

Dkt. Bahati Msaki Mganga Mfawidhi kutoka hospital ya Sekou Toure Mwanza ameishukuru Taasisi ya CHAI kwa kuendelea kuwajengea uwezo wahandisi na mafundi sanifu vifaa tiba katika hospital hapa nchini.

Wahandisi wa vifaaa tiba na wataalam wa Afya nchini wanalojukumu la kulinda na kutunza vifaa tiba vilivyopo nchini ili kuisaidia  serikali kupunguza adha na gharama za Matengezo ya vifaa hivyo.







Post a Comment

Previous Post Next Post