WAKANDARASI MNAOJENGA MINARA YA MAWASILIANO NCHI NZIMA KAMILISHENI MIRADI KWA WAKATI-ENG. KUNDO



WAKANDARASI MNAOJENGA MINARA YA MAWASILIANO NCHI NZIMA KAMILISHENI MIRADI KWA WAKATI-ENG. KUNDO


Na,Mwandishi wetu

Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari imewataka wakandarasi wote nchi nzima wanaojenga miradi ya mawasiliano  kukamilisha miradi hiyo kwa wakati na ifikapo mwaka 2025 mwezi wa tano ujenzi wa minara yote 758 iwe imekamilika.

Hayo yamebainishwa na Naibu Waziri wa wizara hiyo Eng. Kundo Methew katika ziara yake ya kikazi katika baadhi ya Mikoa hapa nchini ambapo amesema kukamilika kwa wakati miradi hiyo watanzania hawatomuuliza Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan swali lolote kuhusu Mawasiliano.

"Tunataka Dkt. Samia Suluhu Hassan akiingia Kwenye uchaguzi 2025 watanzania wasimuulize swali lolote kuhusu Mawasiliano na haya ndiyo tunayoyataka katika Wizara yetu". Amesema Eng. Kundo

Sambamba na hayo Eng. Kundo ameielekeza kampuni ya MTITIMA inayojenga mradi wa jengo jipya la kituo cha Mkongo wa Taifa wilayani Ushirombo Mkoani Shinyanga kuhakikisha ifikapo tarehe 29.2.2024 mradi huo uwe imekamilika.


Naibu waziri wa Habari,Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Eng. Kundo Methew anaendelea na ziara yake ya kikazi katika Mikoa mbalimbali hapa Nchini kwa lengo la kukagua ujenzi wa miundombinu ya mawasiliano.



Picha za matukio mbalimbali zinazoonesha Naibu waziri Eng. Kundo katika ziara yake ya kikazi.




















Post a Comment

Previous Post Next Post