KAMPUNI YA TIGO NA TCDC IMEONGEZA MUDA WA MKATABA WA MAKUBALIANO (MOU) KWA LENGO LA KUWAFIKIA WAKULIMA WOTE NCHINI
Na,Saleh Lujuo-Dodoma
Kampuni ya Tigo nchini kupitia jukwaa la Tigo Pesa imeongeza muda wa Mkataba wake wa Makubaliano (MOU) na Tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania (TCDC) Kwa lengo la Kuimarisha uongezaji wa malipo ya mazao kwa wakulima pamoja na kuimarisha ulizi wa Fedha za wakulima hao.
Akizungumza Mara baada ya Hafla ya utiaji saini Mkataba huo Leo jijini Dodoma, Afisa Mkuu wa Tigo Pesa Bi. Angelica Pesha amesema wakulima wa zao la biashara kulipwa kupitia Tigo Pesa njia salama na rahisi na itaongeza ulinzi wa fedha zao.
Aidha,Bi.Pesha amesema dhamira ya kampuni ya Tigo ni kuimarisha sekta ya kilimo nchini na kuwafanya wakulima kuishi katika Mifumo ya kidigital.
"Sisi kama Kampuni ya Tigo tumeona tuingie makubaliano haya na yanaashiria u Moja, ushirikiano na juhudi za pamoja za kuimarisha ujumuishaji wa kifedha na kuwawezesha wakulima wetu kihifadhi Fedha zao kupitia Tigo Pesa". amesema.
Sambamba na hayo, Bi.Tesha amesema kwa mwaka 2023 kampuni ya Tigo imelipa Takribani Billion 20 kwa wakulima.
Kwa upande wake Mrajisi wa vyama vya Ushirika na Mtendaji Mkuu wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika Dkt. Benson Ndiege amesema makubaliano hayo ni njia pekee itakayowasaidia wakulima kurahisisha malipo na usalama wa fedha zao.
"Tumekuwa tukipata changamoto ya wizi na ubadhirifu wa fedha za wakulima wakiwa wanalipana hivyo mfumo huu wa Tigo Pesa utarahisiaha sana wakulima kulipana kwa urahisi bila kudhulumiana". Amesema
Kampuni ya Tigo nchini imeendelea kuunga mkono Jitihada za serikali ya awamu ya sita Katika kuwawezesha wakulima pamoja na kuchangia ukuaji wa sekta ya kilimo nchini Tanzania.
Tags:
Habari