PPRA IMEWAFUTA MACHOZI WAATHIRIKA WA HANANG KWA KUTOA MILLION 16.1

 


PPRA IMEWAFUTA MACHOZI WAATHIRIKA WA HANANG KWA KUTOA MILLION 16.1

Na,Mwandishi wetu

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu ( Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. Jenista Mhagama ameupongeza Uongozi wa Chama cha Wafanyakazi wa Mamlaka ya Udhibiti wa ununuzi wa Umma (PPRA) kwa kutambua na kuungana na Serikali katika kuwashika mkono waathirika wa maafa ya Maporomoko ya Tope na Mawe ya Hanang Mkoani Manyara kuchangia kiasi cha Shilingi Milioni 16.1 ambazo wamekabidhi hii leo tarehe 28 Disemba, 2023 katika Ofisi ya Waziri Mkuu Jijini Dodoma.

Akizungumza mara baada ya kupokea misaada hiyo Mhe. Mhagama amewashukuru kwa namna walivyochangia fedha hizo huku akiendelea kutoa wito kwa wadau na wananchi kuendelea kuchangia hasa vifaa vinavyoweza kusaidia katika zoezi la kurejesha hali ikiwemo vifaa vya ujenzi

"Kipekee nawashukuru watumishi wote wa PPRA kwa mchango wenu na niwahakikishie utatumika kama ilivyokusudiwa," alisema Mhe. mhagama

Aidha ameeleza kuwa kwa sasa Serikali inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan  inaendelea na zoezi muhimu la kurejesha hali kwa wana Hanang ili kuwapa maisha yenye ubora na furaha na kuhakikisha Watanzania wenzetu wanaendelea na shughuli zao za kujiletea maendeleo kama ilivyopaswa kuwa.

Post a Comment

Previous Post Next Post